Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema mafundisho ya Imam Khomeni MA ndio ramani ya njia ya taifa lililojaa matumaini la Iran na kwamba kuna udharura wa kukabiliana na upotoshaji shakhsia ya Imam.
2015 Jun 04 , 22:55
Siku ya Alkhamisi ya tarehe 4 Juni inasadifiana na kumbukumbu za siku ya kufariki dunia Imam Khomeini MA, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
2015 Jun 04 , 00:17
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema madola ya kigeni na kibeberu hayataweza kuilazimisha Syria ifuate matakwa yao.
2015 Jun 02 , 14:11
Mwenyekiti wa Maulamaa wa Ahlu Sunna nchini Iraq amesema kupambana na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) ni wajibu kwa mujibu wa sheria za Kiislamu.
2015 Jun 02 , 14:06
Walimwengu wanaendelea kulaani hujuma ya kundi la kigaidi na Kitakfiri la ISIS au Daesh dhidi ya msikiti wa Msikiti wa Imam Hussein AS katika mji wa Dammam mashariki mwa Saudi Arabia.
2015 May 30 , 15:34
Mtoto Mwislamu mwenye umri wa miaka miwili amepigwa risasi na kuumizwa vibaya kichwani katika mji wa Bradford nchini Uingereza.
2015 May 18 , 07:54
Jameel Syed, mwanaharakati Mwislamu wa jimbo la Michigan nchini Marekani amekamilisha safari yake ya siku 35 ya kuzunguka na kusoma adhana katika majimbo yote 50 ya nchi hiyo.
2015 May 11 , 06:13
Wabunge 13 Waislamu wamechaguliwa katika uchaguzi wa hivi karibuni nchini Uingereza na hivyo kuweka rekodi mpya iliyoongezeka kutoka wabunge 8 mwaka 2010.
2015 May 09 , 20:15
Mamilioni ya wananchi Waislamu wa Iran wameandamana kote nchini baada ya Sala ya Ijumaa kulaani jinai za utawala wa Saudia dhidi ya watu wa Yemen. Wananchi katika miji mikubwa kama vile Tehran, Qom, Mashhad na miji mingine 770 kote nchini.
2015 May 09 , 19:27
Kikao cha kumi cha kamati ya kudumu inayohusika na masuala ya utamaduni na habari ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kuhusu nafasi ya vijana na vyombo vya habari katika kudumisha amani na uthabiti katika Ulimwengu wa Kiislamu kimefanyika Dakar, mji mkuu wa Senegal.
2015 Apr 30 , 13:02
Viongozi wa dini mbalimbali wamehudhuria katika msikiti wa Tempe katika jimbo la Arizona nchini Marekani na kulaani vikali hatua ya kundi la kibaguzi na linalopiga vita Uislamu ya kuvunjia heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani.
2015 Apr 23 , 14:12
Kiongozi wa ngazi ya juu wa Kiislamu nchini Ufaransa amesema kuwa misikiti 2200 nchini humo haiwatoshelezi mamilioni ya Waislamu wa Ufaransa na kutaka kuongezwa mara mbili idadi ya misikiti iliyopo katika muda wa miaka miwili.
2015 Apr 06 , 18:29
Katika ujumbe wake uliotolewa kwa mnasaba wa kuanza mwaka mpya wa 1394 Hijria Shamsia, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amelitakia heri na mwaka mpya taifa la Iran na mataifa yote yanayoadhimisha sikukuu ya Nowruz na kuupa mwaka mpya jina la Mwaka wa Serikali na Wananchi, Ushirikiano na Mwelekeo Mmoja.
2015 Mar 21 , 04:35