IQNA

Waislamu Ufaransa wataka kujengwa misikiti zaidi

18:29 - April 06, 2015
Habari ID: 3099046
Kiongozi wa ngazi ya juu wa Kiislamu nchini Ufaransa amesema kuwa misikiti 2200 nchini humo haiwatoshelezi mamilioni ya Waislamu wa Ufaransa na kutaka kuongezwa mara mbili idadi ya misikiti iliyopo katika muda wa miaka miwili.

Dalil Boubakeur, Mkuu wa Baraza la Waislamu wa Ufaransa ambaye pia ni mkuu wa msikiti mkuu wa Paris ameyasema hayo juzi katika mji wa Le Bourget karibu na mji mkuu huo kwenye mkutano wa muungano wa taasisi za Kiislamu za Ufaransa (UOIF), unaozikutanisha pamoja taasisi za Kiislamu zaidi ya 250.
Mkuu wa msikiti mkuu wa mjini Paris amesema kuwa, ipo haja ya kuongezwa maradufu idadi ya misikiti ya sasa ya Ufaransa katika muda wa miaka miwili ili kukidhi mahitaji ya Waislamu walioko nchini humo. Naye Amar Lasfar, Mkuu wa muungano wa taasisi za Kiislamu za Ufaransa (UOIF), ameunga mkono ombi la mkuu wa msikiti mkuu wa Paris akisema kuwa, idadi ya misikiti huko Ufaransa inapasa kuakisi idadi ya Waislamu waishio nchini humo. Amesema Waislamu wana haki ya kujenga misikiti na kwamba jambo hilo halipasi kupingwa na mameya wa miji.../mh

3085074

captcha