Tafsiri ya Kiingereza ya Qur'ani Tukufu iliyoandikwa kwa Braille (maandishi makhsusi kwa ajili ya vipofu) imechapishwa kwa mara ya kwanza na mtafiti na mtaalamu wa Qur'ani nchini Uturuki.
2011 Feb 26 , 09:35
Hatua za mwisho za kutarjumi na kutafsiri baadhi ya aya za Qur'ani kwa lugha ya ishara zimekamilika katika Kituo cha Qur'ani cha Mfalme Fahd katika mji mtakatifu wa Madina.
2011 Feb 24 , 12:18
Nuskha adimu za Qur'ani Tukufu zitaonyeshswa na kuuzwa kupitia mnada tarehe 5 na 6 za mwezi ujao wa Machi huko Doha mji mkuu wa Qatar.
2011 Feb 24 , 12:09
Madrasa ya kwanza ya Qur'ani imeanzishwa katika mji wa Burama nchini Somalia kwa hima ya Taasisi ya Masuala ya Kheri ya nchi hiyo.
2011 Feb 23 , 14:37
Benki ya Kiislamu ya Dubai DIB imetangaza kwamba mwaka huu pia itadhamini mashindano ya Qur'ani ya Ras al-Khaimah.
2011 Feb 23 , 11:27
Shughuli za kuadhimisha duru ya 12 ya Wiki ya Kitaifa ya Qur'ani zilianza jana Jumatatu katika kituo cha kidini cha Dar al-Imam katika mji wa Algiers nchini Algeria.
2011 Feb 22 , 16:25
Kitengo cha shughuli za vijana cha Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Turathi ya Qatar kinajitayarisha kuandaa duru ya 24 ya mashindano ya Qur'ani Tukufu na hadithi za Mtume kwa vijana wa nchi hiyo.
2011 Feb 22 , 16:20
Majlisi ya sita ya kiraa ya Qur'ani Tukufu ya wasomaji mashuhuri wa nchi za kandokando ya Ghuba ya Uajemi itafanyika tarehe 24 Februari katika mji wa Waislamu wengi wa Kishia wa Saihat huko mashariki mwa Saudi Arabia.
2011 Feb 20 , 14:06
Mashindano ya sita ya kuhifadhi Qur'ani tukufu yamepangwa kufanyika tarehe 27 Februari katika Kituo cha Kiislamu cha Virginia (CVQC) katika mji wa Richmond huko Marekani.
2011 Feb 19 , 17:05
Kitabu cha Masomo ya Msingi ya Kiraa Sahihi ya Qur'ani kimechapishwa katika mji mtakatifu wa Qum chini ya usimamizi wa Kituo cha Qur'ani cha Hadhrat Ruqayyah (as).
2011 Feb 17 , 10:46
Mashindano ya kitaifa ya qiraa ya Qur'ani Tukufu yamefanyika India katika mji mkuu wa Uttar Pradesh, Lucknow mnamo Februari 14.
2011 Feb 17 , 10:24
Sayyid Hamed Malakuti Tabar, Mwambata wa Utamaduni wa Iran huko Sudan amekutana na Suleiman Othman Mkuu wa Chuo Kikuu cha Qur'ani nchini humo na wameafikiana kuimarisha uhusiano wa nchi mbili katika masuala ya Qur'ani.
2011 Feb 17 , 10:20
Muungano wa Waislamu wa Canada na Kituo cha Habari cha Kiislamu vitafanya mashindano ya 10 ya Qur'ani katika jimbo la British Columbia nchini Canada.
2011 Feb 16 , 17:21