Walimu wa vituo na taasisi za Qur'ani kutoka miji tofauti ya Iraq wamekutana katika mji mtakatifu wa Karbala kwa ajili ya kujadili njia za kutatua matatizo yaliyopo kuhusiana na njia za kufundisha kitabu hicho kitakatifu.
2011 Mar 06 , 18:25
Nuskha ya maandishi ya mkono ya Qur'ani Tukufu yenye umri wa miaka 1000 iliyopatikana mkoani Shandong mwaka 2008 sasa inasubiri msaada wa serikali ya China kwa ajili ya kutayarishiwa jumba maalumu la makumbusho mahala itakapohifadhiwa.
2011 Mar 06 , 18:01
Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu na Hadithi za Mtume (saw) yaliyopewa jina la Muhammad bin Jalwi yamepangwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 5 Machi katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.
2011 Mar 03 , 12:09
Kongamano la kwanza la kitaifa yenye anwani ya ‘Afya kwa Mtazamo wa Qur'ani’ limeanza Machi 2 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Razi mjini Tehran.
2011 Mar 02 , 20:03
Wafungwa karibu 250 katika jumbo la Zamfara nchini Nigeria wamefanikiwa kukamilisha mafunzo ya kiraa ya Qur'ani Tukufu na mbinu mbalimbali za kiraa kutoka kwa wataalamu wa mada hiyo.
2011 Mar 01 , 16:06
Duru ya 24 ya mashindano ya kitaifa ya Qur'ani na Hadithi maalumu kwa vijana wanachama wa vilabu vya michezo na vituo vya utamaduni vya Qatar yalianza nchini humo siku ya Jumapili tarehe 27 Februari.
2011 Mar 01 , 14:53
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, akizungumza katika sherehe za kuzindua zulia lenye thamani kubwa lililonakshiwa juzuu zote 30 za Qur'ani Tukufu, amesema kwamba sanaa ni matunda ya kazi za mwanaadamu.
2011 Mar 01 , 09:02
Warsha ya kwanza ya kitaifa yenye anwani ya ‘Afya kwa Mtazamo wa Qur'ani’ itafanyika kuanzia Machi 2-3 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Razi mjini Tehran.
2011 Feb 28 , 11:13
Kozi ya msingi ya qiraa ya Qur'ani Tukufu maalumu kwa wanaume inafanyika nchini Australia kwa himaya ya Akademia ya Sayansi na Utafiti wa Kiislamu Australia ISRA.
2011 Feb 27 , 15:16
Nabil Abdul Aziz al-Hammad mkuu wa kanali ya satalaiti ya Ahlul Qur'an ambayo inafungamana na Jumuiya ya Kimataifa ya Hifdh al-Qur'an ametanagaza habari ya kufunguliwa rasmi hivi karibuni televisheni hiyo ya satalaiti.
2011 Feb 26 , 15:25
Duru ya sita ya mahfali ya kimataifa ya usomaji Qur'ani Tukufu ambayo imewajumuisha wasomaji mashuhuri wa Qura'ni kutoka nchi za Ghuba ya Uajemi imefanyika huko katika mji wa wakazi wengi wa Kishia wa Seihat nchini Saudi Arabia.
2011 Feb 26 , 15:23
Awamu ya mwisho ya mashindano ya 18 ya kuhifadhi Qur'ani na hadithi za Mtume (saw) ya wanafunzi wa shule za msingi itaanza kesho Jumapili katika mji wa Riyadh nchini Saudi Arabia.
2011 Feb 26 , 09:39
Tafsiri ya Kiingereza ya Qur'ani Tukufu iliyoandikwa kwa Braille (maandishi makhsusi kwa ajili ya vipofu) imechapishwa kwa mara ya kwanza na mtafiti na mtaalamu wa Qur'ani nchini Uturuki.
2011 Feb 26 , 09:35