Kauli mbiu ya maonyesho ya 19 ya Qurani Tukufu ya Tehran imetangazwa kuwa ni ‘Qurani, Kitabu cha Mwamko wa Kiislamu’.
2011 Apr 06 , 15:37
Kikao cha pili cha Utafiti wa Kiislamu kimepangwa kufanyika tarehe 16 na 17 za mwezi Julai huko katika mji wa Oxford nchini Uingereza.
2011 Apr 05 , 17:46
Hatua ya pili ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu kwa watoto, ambayo yameandaliwa na televisheni ya watoto ya al-Jazeera kwa ushirikiano wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar yalianza nchini humo hapo jana Jumatatu tarehe 4 Aprili.
2011 Apr 05 , 17:45
Kikao cha kupanga mikakati ya Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qurani kimefanyika Aprili nne mjini Tehran.
2011 Apr 05 , 10:39
Mashindano ya Kimataifa ya Qurani ya Kuwait yamepangwa kuanza Jumatano Aprili 13 katika mji mkuu wa nchi hiyo Kuwait City.
2011 Apr 04 , 00:36
Kongamano la kimataifa la mafunzo kwa wakuu wa taasisi za Qur'ani limepangwa kufanyika hapo kesho Jumatatu tarehe 4 hadi Jumatano tarehe 6 Aprili huko Khartoum , mji mkuu wa Sudan.
2011 Apr 03 , 17:53
Waalimu 76,000 wa Qurani Tukufu wameshiriki na kufuzu katika kozi maalumu za mafundisho ya Qurani zilizofanyika katika mkoa wa Tehran nchini Iran kuanzia Macho 2010 hadi Machi 2011.
2011 Apr 03 , 13:31
Mashindano ya Kitaifa ya Qurani kwa ajili ya Vikosi vya Kijeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yatafanyika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mei 17-18.
2011 Apr 03 , 13:30
Idara Kuu ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Imarati siku ya Jumanne iliandaa masomo maalumu kwa ajili ya Mahafidh wa Qur'ani Tukufu huko katika Msikiti wa Muhammad bin Zayed katika mji mkuu Abu Dhabi.
2011 Mar 31 , 11:36
Washiriki wa sherehe za kuwaenzi washindi wa mashindano ya kimataifa ya muujiza wa kielimu wa Qur'ani na sunna za Mtume Mtukufu (saw) ambazo zilifanyika hapo siku ya Jumanne huko katika mji mkuu wa Misri Cairo, wametaka kuasisiwa kwa chuo cha muujiza wa kielimu wa Qur'ani nchini humo.
2011 Mar 31 , 11:35
Sayyid Yusuf Ridha Gilani, Waziri Mkuu wa Pakistan amesema kuwa dharau iliyofanyiwa Qur'ani Tukufu kwa kuchomwa moto katika kanisa moja huko katika jimbo la Florida nchini Marekani inabainisha wazi mielekeo ya kuvuka mipaka katika baadhi ya jamii.
2011 Mar 29 , 11:13
Wakizungumza kwa njia ya simu, Marais Asif Ali Zardari wa Pakistan na Abdallah Gul wa Uturuki wamechunguza dharau iliyofanywa hivi karibuni dhidi ya kitabu kitakatifu cha Qur'ani katika mojawapo ya makanisa ya Jimbo la Florida huko Marekani.
2011 Mar 29 , 10:48
Rahman Malik, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan ameiandikia barua polisi ya kimataifa ya Interpol akiitaka ifuatile kwa karibu wahalifu waliohusika na uchomaji Qur'ani Tukufu huko katika jimbi la Florida nchini Marekani.
2011 Mar 29 , 10:47