Haram ya Imam Hussein bin Ali (as) katika mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq itakaribisha wasomaji mashuhuri wa Qur'ani kutoka maeneo mbalimbali duniani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
2011 Jun 14 , 16:47
CD za vitabu na athari za mfasiri mashuhuri wa Qur'ani wa Misri marehemu Muhammad Mutawalli al Sha'rawi itatolewa mjini Cairo.
2011 Jun 14 , 16:45
Idara ya Utamaduni ya Iran nchini Tanzania imenadaa mashindano ya Qur'ani katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
2011 Jun 14 , 15:33
Kongamano la pili la kuwaenzi wanawake wanaharakati wa Qur'ani Tukufu nchini Iran litafanyika tarehe 27 Rajab kwa mnasaba wa kukumbuka siku ya Kubaathiwa na kupewa utume Nabii Muhammad SAW.
2011 Jun 14 , 15:29
Wanafunzi wa mashindano ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani Tukufu huko Bahrain walishukuriwa na kuenziwa katika sherehe maalumu iliyofanyika katika shule ya Kiislamu ya Ibn Haitham hapo siku ya Jumapili katika mji mkuu wa nchi hiyo Manama.
2011 Jun 13 , 17:33
Duru ya sita ya mashindano ya kimataifa ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani Tukufu yaliyopewa jina la al-Hashimi maalumu kwa wanawake wa Kiislamu yalianza jana Jumapili huko Amman nchini Jordan.
2011 Jun 13 , 17:28
Mashindano ya 54 ya taifa ya Qur'ani ya Malaysia yanatazamiwa kuanza leo usiku yakihudhuriwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Najib Tun Razzak. Mashindano hayo yanafanyika katika mji wa Kuching katika jimbo la Sarawak.
2011 Jun 13 , 16:11
Shirika la Awqaf na Misaada la Iran huandaa mashindano zaidi ya 1,600 ya Qur'ani kila mwaka nchini Iran katika viwango mbalimbali.
2011 Jun 13 , 14:59
Walimu 500 wamefuzu kutoa mafunzo ya Qur'ani kwa walimu wa darasa la nne katika shule za msingi nchini Iran.
2011 Jun 13 , 14:27
Nakala za maandishi ya mkono na za kale za Qur'ani Tukufu zinazojumuisha tarjumi za kitabu hicho kitukufu zinaonyeshwa katika mji wa Karachi nchini Pakistan.
2011 Jun 12 , 17:51
Taasisi ya Masuala ya Kheri na Kiislamu ya Dubai imepanga kufanya kikao maalumu siku ya Ijumaa tarehe 17 Juni kwa shabaha ya kujadili na kujibu maswali kuhusiana na mambo yasiyofahamika vyema na fikra potofu kuhusiana na baadhi ya mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
2011 Jun 12 , 15:06
Uandikishaji wa majina ya washiriki wa mashindano ya kwanza ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu kwa walemavu wa akili ulianza hapo jana Jumamosi nchini Misri. Mashindano hayo yameandaliwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya nchi hiyo.
2011 Jun 12 , 14:57
Kituo cha Kiislamu cha Uingereza kimeanza kutoa mafunzo ya kitabu kitakatifu cha Qur’ani kwa watu waliosilimu wanaoishi nchini humo.
2011 Jun 11 , 21:12