Mahafidhi wa Darul Qur'ani ya Haram ya Imam Hussein (as) katika mji mtakatifu wa Karbala jana walishiriki katika shughuli ya kuomboleza mauaji ya mjukuu huyo wa Mtume Muhammad (saw).
2011 Dec 07 , 18:02
Mashindano ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani ya Sheikh Ghanim ya wanawake nchini Qatar yanaanza leo baada ya mashindano kama hayo ya wanaume kuvutia watu wengi.
2011 Dec 04 , 09:09
Maonyesho ya nakala ya Qur'ani Tukufu yenye umri wa miaka 300 yamewavutia watu wengi katika mji wa Jeddah nchini Saudi Arabia.
2011 Dec 03 , 18:00
Sherehe za kuwaenzi washindi wa mashindano ya kiraa ya Qur'ani makhsusi kwa ajili ya watoto itafanyika tarehe 6 Disemba katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.
2011 Dec 03 , 17:59
Imepita miaka 23 sasa tangu karii na msomaji mashuhuri wa Qur'ani Tukufu Ustadh Abdul Basit Abdus Samad alipoaga dunia katika ardhi ya nchi ya Misri ambayo kwa sasa inapita katika kipindi cha mabadiliko makubwa ya kuelekea kwenye demokrasia baada ya kung'olewa madarakani utawala wa kidikteta wa Hosni Mubarak mapema mwaka huu.
2011 Nov 30 , 19:52
Masomo ya muda ya sheria na kanuni za kiraa na tajwidi ya Qur'ani Tukufu yalianza jana Jumanne katika mji wa Nablos huko Palestina kwa hima ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya kidini.
2011 Nov 30 , 17:00
Kituo cha Qur'ani Tukufu kwa jina la Ali bin Hussein as-Sada maalumu kwa wanawake, kilifunguliwa jana Jumatatu katika mji wa Shimal nchini Qatar kwa ufadhili wa Idara ya Uhubiri na Mwongozo wa Kidini ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya nchi hiyo.
2011 Nov 29 , 16:11
Wanachuo wa Kiislamu wa somo la tiba wa Chuo Kikuu cha London wameondoka darasani kama hatua ya kupinga nadharia ya Charles Darwin kuhusu mabadiliko ya maumbile ya mwanadamu (Theory Of Evolution) kutokana na nadharia hiyo kupingana na mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
2011 Nov 28 , 17:06
Vikao vya mafunzo ya kuzingatia Qur'ani Tukufu vitaanza kufanyika tarehe 2 Disemba katika mji wa Manchester kwa hima ya Jumuiya ya Kiislamu ya chuo kikuu cha mji huo.
2011 Nov 28 , 16:37
Jumuiya ya Kulinda Qur'ani Tukufu ya Jordan imechaguliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu kuwa mshindi wa Tuzo ya Kimataifa ya Kuhudumia Qur'ani Tukufu katika mwaka 2011.
2011 Nov 28 , 16:16
Kundi moja la wafanyaziara wa Kiirani wameikabidhi Haram ya Imam Hussein (as) nuskha moja ya Qur'ani Tukufu ambayo imeandikwa kwa mkono kwa ushirikiano wa wasanii 1000 wa Iran.
2011 Nov 28 , 15:07
Programu iliyopewa jina la ‘Lango la Amani: Utambuzi wa Uislamu, Qur’ani na Mtume Muhammad (saw) itafanyika tarehe 29 Novemba katika Chuo Kikuu cha Missouri nchini Marekani.
2011 Nov 27 , 23:52
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kiislamu ya Dubai amesema kuwa imeundwa tena kamati maalumu ya kuchapisha na kusambaza Msahafu wa Kitaifa wa Imarati kwa jina la Msahafu wa Sheikh Maktoum bin Rashid Aal Maktoum.
2011 Nov 27 , 16:57