Tafsiri ya sura tukufu ya Hud imepangwa kuchunguzwa hivi karibuni katika Chuo cha Queen Mary katika Chuo Kikuu cha London.
2011 Dec 28 , 15:39
Kongamano la Mchango wa Vyombo vya Habari katika Kueneza Utamaduni wa Qur'ani nchini Iraq utafanyika kesho katika mji wa Nasiriyya kwa ushirikiano wa Shirika la habari la IQNA.
2011 Dec 27 , 22:22
Mashindano ya 12 ya Qur'ani Tukufu yamepangwa kufanyika mwezi Machi mwakani katika Kituo cha Kiislamu cha Masumeen kwenye eneo la New England huko Marekani.
2011 Dec 26 , 10:43
Taasisi ya Mambo ya Kheri ya Yumn ya Misri imetoa wito wa kukusanywa nuskha za Qur'ani Tukufu zisizotumika majumbani kwa ajili ya kutumwa katika nchi tofauti za kusini mwa Afrika.
2011 Dec 26 , 10:36
Maonyesho ya kaligrafia na kazi za wasanii wa Pakistan zinazohusu maudhui za aya za Qur'ani imeanza katika mji wa Lahore.
2011 Dec 25 , 14:59
Sherehe za kuhitimisha duru ya tatu ya mashindano ya kimataifa ya hifdhi, tajwidi na tafsiri ya Qur'ani Tukufu zimepangwa kufanyika leo Jumapili katika Masjidul Haram nchini Saudi Arabia.
2011 Dec 25 , 11:58
Mashindano ya hifdhi ya Qu'ani Tukufu makhsusi kwa ajili ya watoto wadogo yatafanyika tarehe 20 Aprili mwakani katika jimbo la Vermont nchini Marekani.
2011 Dec 20 , 17:58
Maonyesho ya Qur'ani Tukufu kuhusu sanaa yamefanyika katika mji wa Cranbourne katika jimbo la Victoria nchini Australia.
2011 Dec 20 , 16:20
Nuskha 170,000 za Qur'ani Tukufu zimegawiwa kwa washiriki wa kongamano la kimataifa la Qur'ani Tukufu lililomalizika hivi karibuni mjini Khartoum, Sudan.
2011 Dec 19 , 22:50
Kituo cha kwanza cha Qur'ani cha Kishia kimefunguliwa katika mji wa Guangzhou nchini Uchina.
2011 Dec 19 , 08:12
Mashindano ya 33 ya kimataifa ta hifdhi, tajwidi na tafsiri ya Qur'ani yamenza leo nchini Saudi Arabia chini ya usimamizi wa Wizara ya Wakfu, Tablighi na Miongozo ya nchi hiyo. Mashindano hayo yanafanyika katika Masjidul Haram mjini Makka.
2011 Dec 18 , 12:35
Mashindano ya 28 ya Qur'ani Tukufu yatafanyika Jumatatu ijayo katika Msikiti wa Faisal Abad katika mkoa wa Punjab nchini Pakistan.
2011 Dec 17 , 18:56
Watafiti kadhaa wa utamaduni wa Kiislamu nchini China wamegundua tarjumi ya kwanza ya Qur'ani Tukufu iliyoandikwa kwa mkono. Tarjumi hiyo ni ya lugha ya Kichina.
2011 Dec 17 , 16:13