Mpango wa kukusanya nakala milioni moja za Qur'ani Tukufu kwa ajili ya bara la Afrika umeanza kutekelezwa nchini Bahrain kwa hima ya Jumuiya ya Vyombo vya Habari vya nchi hiyo.
2012 Jan 28 , 17:51
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Morocco yalimalizika jana kwa washindi kutunukiwa zawadi.
2012 Jan 28 , 17:20
Masomo ya elimu ya kiraa ya Qur'ani Tukufu yalianza jana katika mji mkuu wa Mauritania, Nouachott.
2012 Jan 28 , 16:49
Mafunzo maalumu ya Ta’alumul Qur’ani kwa waliosilimu katika Jeshi la Kifalme la Brunei yatamalizika Jumapili 29 Januari.
2012 Jan 28 , 16:24
Kongamano la kimataifa la Uchunguzi wa Vizuizi vya Mafunzo ya Qur’ani Tukufu limepangwa kufanyika tarehe 28 mwezi huu wa Januari nchini Misri chini ya usimamizi wa Baraza la Kiislamu la Kimataifa.
2012 Jan 25 , 18:44
Mafunzo ya muda ya Siri za Qur’ani yatatolewa kwa kipindi cha wiki 12 katika Chuo Kikuu cha Irfan na Tiba ya Kiroho (USHS) katika mji wa Angwin nchini Marekani.
2012 Jan 25 , 18:44
Walimu na wasimamizi wa shule za Qur'ani nchini Senegal wameitaka serikali ya nchi hiyo kutazama upya sheria zinazohusiana na masuala ya madrasa za Qur'ani Tukufu.
2012 Jan 23 , 17:30
Sira na maisha ya hafidhi asiyeona wa Qur'ani Tukufu wa Pakistan yatachunguzwa katika kongamano litakalofanyika kwa ushirikiano wa ubalozi wa Pakistan nchini Bahrain chini ya usimamizi wa Kituo cha Utafiti wa Masuala ya Kiutamaduni na Elimu za Kiislamu Marekani na Canada.
2012 Jan 23 , 17:30
Mashindano ya tatu ya kitaifa ya hifdhi ya Qur’ani yaliyopewa jina la Tuzo ya Khalifa bin Jabir yatafanyika tarehe 26 Januari nchini Imarati.
2012 Jan 22 , 14:21
Taasisi ya Kimataifa ya Qur'ani, Zawadi ya Dubai, imetangaza kuwa hatua ya mwanzo ya duru ya 13 ya mashindano ya kitaifa ya Qur'ani, Zawadi ya Dubai imeakhirishwa na kusema kwamba sasa yatafanyika tarehe 21 mwezi huu wa Januari.
2012 Jan 16 , 14:58
Jamhuri ya Tatarstan katika Shirikisho la Russia imetangaza mwaka 2012 kuwa ‘Mwaka wa Qur’ani Tukufu.
2012 Jan 15 , 14:31
Msahafu mkubwa zaidi ulioandikwa kwa mkono umezinduliwa katika sherehe iliyohudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa kidini na kiserikali mjini Kabul, Alkhamisi iliyopita.
2012 Jan 15 , 11:56
Muhammad Qaim Swafa Fumi Sawada, Mwislamu wa Kishia wa Japan ambaye ni mtarjumi wa Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kijapani na ambaye ameandika vitabu kadhaa vya Kiislamu na Kishia ameaga dunia.
2012 Jan 11 , 12:34