Waislamu nchini Russia hasa katika jimbo la Tatarstan wanapanga kuadhimisha 'Mwaka wa Qur'ani' mwaka huu wa 2012 kwa mnasaba wa mwaka wa 225 tokea ichapishwe Qur'ani ya kwanza iliyotarjumiwa kwa Kirusi.
2012 Feb 05 , 15:57
Juzuu ya 30 ambayo ni juzuu ya mwisho ya Qur'ani Tukufu imetajumiwa kwa lugha nne za Kiafrika kwa udhamini wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamduni wa Kiislamu ISESCO.
2012 Feb 05 , 11:20
Awamu ya mwisho ya Olimpiadi ya 17 ya Qur'ani na Hadithi kwa ajli ya wanachuo wa kigeni nchini Iran katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa itaanza kesho Februari 5.
2012 Feb 04 , 14:27
Duru ya 12 ya mashindano ya hifdhi, kiraa na tafsiri ya Qur'ani Tukufu maalumu kwa vilema wa viungo vya mwili, yaliyopewa jina la Zawadi ya Ra'sul Kheima yalianza siku ya Jumanne katika ufalme huo unaounda Umoja wa Falme za Kiarabu.
2012 Feb 02 , 12:18
Masomo ya muda mfupi ya tajwidi ya Qur'ani Tukufu yamepangwa kufanyika hivi karibuni katika Msikiti wa Hamad bin Khalid mjini Doha Qatar ambapo mahafidh mashuhuri wa Qur'ani kutoka kila pembe za nchi hiyo wanatazamiwa kushiriki.
2012 Feb 02 , 12:16
Qur'ani iliyoandikwa kwenye bao ilionyeshwa siku ya Jumatatu pambizoni mwa kikao cha saba cha Baraza Kuu la Muungano wa Mabunge ya Kiislamu katika mji wa Palampang, Indonesia.
2012 Feb 01 , 17:02
Baraza la Kitaifa la Vyombo vya Habari la Imarati limekusanya nakala za Qur'ani zilizo na makosa ya chapa kutoka soko la mji wa al-Ain.
2012 Feb 01 , 17:02
Msahafu wa kitaifa wa Imarati umechapishwa upya katika mwaka huu wa 1433 Hijiria kwa udhamini wa Idara Kuu ya Masuala ya Kiislamu na Wakfu ya nchi hiyo.
2012 Jan 31 , 12:17
Taasisi ya Qur'ani Tukufu inayofungamana na Haram ya Hadhrat Abbas (as) nchini Iraq inafuatilia suala la kuanzisha matawi yake katika mikoa mbalimbali ya nchi hiyo ukiwemo mji wa Arbil katika jimbo linalojitawala la Kurdestan.
2012 Jan 30 , 17:26
Washindi wa Mashindano ya Qur’ani ya ‘Miladun Nabii’ maalumu kwa vilema yaliyofanyika Misri wataenziwa Februari mosi mjini Cairo.
2012 Jan 30 , 14:45
Semina inayojadili muujiza wa kielimu wa Qur'ani Tukufu iliyofanyika chini ya anwani ya 'Damu iliyoko kwenye Mishipa ya Mwanadamu ni Dalili ya Kuwepo Mwenyezi Mungu' ilifanyika jana Jumamosi tarehe 28 nchini Jordan.
2012 Jan 29 , 16:20
Mashindano ya kumi ya kitaifa ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu yatafanyika tarehe 8 Aprili nchini Ufaransa kwa hima ya Muungano wa Jumuiya za Kiislamu za Ufaransa.
2012 Jan 29 , 10:40
Mpango wa kukusanya nakala milioni moja za Qur'ani Tukufu kwa ajili ya bara la Afrika umeanza kutekelezwa nchini Bahrain kwa hima ya Jumuiya ya Vyombo vya Habari vya nchi hiyo.
2012 Jan 28 , 17:51