Maadhimisho ya 13 ya Wiki ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu yamepangwa kufanyika katika Kituo cha Kidini cha Dar al Imam katika mji mkuu wa Ageria, Algiers.
2012 Feb 13 , 16:01
Mwanafikra wa Kiislamu ambaye pia ni Imamu wa Swala ya Ijumaa ya mji wa Qatif nchini Saudi Arabia ameitaka Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya nchi hiyo kuzingatia taasisi za kidini na Qur'ani za Mashia wa nchi hiyo.
2012 Feb 12 , 14:56
Maonyesho ya Qur'ani Tukufu yalifunguliwa siku ya Alkhamisi pambizoni mwa mashindano ya Qur'ani Tukufu Zawadi ya Ra's al- Khaima katika Umoja wa Falme za Kiarabu.
2012 Feb 12 , 14:42
Taasisi ya Kimataifa ya 'Kuitafakari Qur'ani' imeanzishwa Februari 8 na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar.
2012 Feb 08 , 21:31
Mashindano yaa hifdhi na kiraa ya Qur’ani Tukufu yamepangwa kufanyika katika Kituo cha Waislamu wa Madhehebu ya Shia Ithnaashari katika eneo la Stanmore nchini Uingereza. Mashindano hayo yatafanyika kwa hima ya Darul Qur’an wal Itra.
2012 Feb 08 , 16:54
Duru ya 11 ya mashindano ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani Tukufu imepangwa kufanyika nchini Canada tarehe 2 Aprili.
2012 Feb 08 , 16:09
Waziri wa Elimu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hamid Ridha Haji Babai amesema walimu 5000 wapya wa Qur'ani wataajiriwa kote nchini.
2012 Feb 06 , 22:03
Wizara ya Masuala ya Kidini Brunei inaandaa Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qur'ani na Tafsiri katika mwaka huu wa 1433.
2012 Feb 06 , 21:59
Duru ya 12 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Russia ilifanyika jana katika mji mkuu wa nchi hiyo Moscow.
2012 Feb 06 , 16:25
Duru ya 13 ya mashindano ya kitaifa ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu Zawadi ya Dubai yanaendelea kufanyika nchini Imarati kwa kuwashirikisha washindani kutoka kila pembe ya umoja huo wa Kiarabu.
2012 Feb 06 , 11:55
Sherehe za kuonyeshwa tarjumi mpya ya Qur'ani kwa lugha ya Kichina ilifanyika jana katika Jumuiya ya Wakfu na Masuala ya Kheri nchini Iran.
2012 Feb 05 , 16:14
Mtarjumi wa kwanza wa tafsiri ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kikurdi nchini Uturuki Mulla Abdullah Farly alifariki dunia jana katika hospitali ya Bin Sina katika mji wa Aghry nchini Uturuki akiwa na umri wa miaka 72.
2012 Feb 05 , 15:58
Waislamu nchini Russia hasa katika jimbo la Tatarstan wanapanga kuadhimisha 'Mwaka wa Qur'ani' mwaka huu wa 2012 kwa mnasaba wa mwaka wa 225 tokea ichapishwe Qur'ani ya kwanza iliyotarjumiwa kwa Kirusi.
2012 Feb 05 , 15:57