Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran ameashiria hatua ya hivi karibuni ya Wamarekani kuivunjia heshima Qur'ani na kusema: 'Waislamu watajibu vikali kitendo hicho cha Wamarekani kwa kushikamana zaidi na Qur'ani'.
2012 Feb 29 , 19:09
Chuo Kikuu cha Birmingham cha Uingereza kinapanga kuandaa mashindano ya Qur'ani kwa wanachuo wa Kiislamu hapo tarehe 14 Machi.
2012 Feb 29 , 15:20
Semina ya 'Muujiza wa Qur'ani; Lugha ya Zama Hizi' imepangwa kufanyika leo Jumatano huko Jordan. Semina hiyo imeandaliwa na Jumuiya ya Miujiza ya Qur'ani na Suna ya Jordan.
2012 Feb 29 , 15:18
Wimbi kubwa la malalamiko ya wananchi wa Afghanistan dhidi ya kitendo kiovu cha askari wa Marekani cha kuchoma moto Qur'ani Tukufu limewalazimisha wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo kuondoka Afghanistan.
2012 Feb 28 , 15:28
Masomo ya muda ya kiraa na tajwidi ya Qur'ani Tukufu yanaendelea kutolewa katika mji mtakatifu wa Karbala kwa hima ya Taasisi ya Qur'ani ya Haram ya Hadhrat Abbas (as) na Msikiti wa al Muntadhar.
2012 Feb 27 , 23:21
Sherehe za kuwaenzi mahafidhi 44 wa Qur'ani nzima zilifanyika siku ya Jumamosi tarehe 25 Februari katika mji wa Tripoli nchini Lebanon.
2012 Feb 27 , 14:50
Mashindano ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu yamepangwa kufanyika tarehe 1 na 2 Aprili katika Chuo cha Dupage katika mji wa Chicago nchini Marekani.
2012 Feb 26 , 16:00
Mwanazuoni mashuhuri wa Lebanon Sheikh Muhammad Namr Zaghmut ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Kiislamu la Palestina nchini Lebanon amekosoa kimya cha watawala wa nchi za Kiarabu mbele ya vitendo vya askari wa Marekani vya kuchoma moto Qur'ani Tukufu na akasisitiza kuwa Waislamu watailinda Qur'ani Tukufu kwa nafsi na roho zao.
2012 Feb 26 , 15:50
Mateka wa Kipalestina walioachiwa huru hivi karibuni kutoka kwenye jela za Israel ambao wamehifadhi Qur'ani Tukufu wameenziwa katika mji wa Rafah huko Gaza kwa hima ya Taasisi ya Darul Qur'ani.
2012 Feb 25 , 17:50
Duru ya 51 ya mashindano ya hifdhi ya Qur'ani tukufu ya wanafunzi yamepangwa kufanyika tarehe 11 Machi katika mji mkuu wa Qatar, Doha.
2012 Feb 22 , 17:44
Baada ya kushadidi malalamiko ya Waislamu wanaopinga kuvunjiwa heshima Qur'ani:
Ubalozi wa Marekani mjini Kabul, Afghanistan umefungwa leo siku mbili tu baada ya askari wa nchi hiyo kuvunjia heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani.
2012 Feb 22 , 17:35
Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imelaani kitendo cha askari wa Marekani nchini Afghanistan cha kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu katika kituo cha jeshi la anga cha Bagram huko kaskazini mwa mji wa Kabul.
2012 Feb 22 , 16:51
Wananchi wa Afghanistan wamefanya maandamano mapema leo mbele ya makao makuu ya askari wa Marekani mjini Kabul wakipinga kitendo cha kuchomwa moto nakala za Qur'ani Tukufu kilichofanywa na wanajeshi wa Marekani.
2012 Feb 21 , 18:31