Nakala ya Qur'ani Tukufu iliyoandikwa kwa hati za mkono mwaka 1112 Miladia inaonyeshwa katika chumba cha Austria katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu mjini Riyadh, Saudi Arabia kwa ajili ya kuuzwa.
2012 Mar 10 , 22:27
Taifa la Kiislamu la Pakistan limejibu kitendo kiovu kilichofanywa na askari wa Marekani cha kuchoma moto Qur'ani Tukufu kwa kutangaza Ijumaa ya jana tarehe 9 Machi kuwa ni Siku ya Adhama ya Qur'ani Tukufu.
2012 Mar 10 , 22:26
Wanakaligrafia wawili wa Iran na Uturuki wanashirikiana katika kuandika nakala ya Qur'ani Tukufu ambayo itakuwa ndefe zaidi duniani.
2012 Mar 10 , 22:26
Bunge la Jimbo la Punjab limepitisha mswada ambao utafanya mafunzo ya Qur'ani Tukufu katika shule zote za jimbo hilo kuwa ya lazima kuanzia mwakani.
2012 Mar 10 , 13:53
Mkuu wa Idara Kuu ya Masuala ya Kiislamu na Kheri ya Dubai ametoa amri ya kuasisiwa mjini humo Kituo cha Hifdhi ya Qur'ani kitakachopewa jina la al-Jabiri.
2012 Mar 05 , 16:26
Mashindano ya 25 ya Qur'ani Tukufu na Hadithi maalumu kwa vijana wa Qatar yalimalizika jana Jumapili nchini humo.
2012 Mar 05 , 16:26
Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema wizara hiyo imeanzisha harakati ya utafiti wa Qur'ani katika setka za tiba na afya.
2012 Mar 05 , 13:41
Nchini Uturuki, wasichana waliohifadhi Qur'ani wameenziwa katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Oovtadh mjini Nuchehar.
2012 Mar 05 , 13:41
Mashindano ya 17 ya kila mwaka ya Qur'ani maalumu kwa vijana wa kiume yatafanyika Septemba pili mwaka huu katika Shule ya Broadway mjini Birmingham Uingereza.
2012 Mar 05 , 13:25
Kituo cha uchapishaji Qur'ani na vitabu ningine vinavyohusiana na kitabu hicho kitakatifu kitajengwa hivi karibuni huko Ajman, ufalme mdogo zaidi kati ya falme saba zinazobuni Umoja wa Falame za Kiarabu au kwa jina jingine Imarati.
2012 Mar 04 , 17:04
Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Jordan ametuma mwaliko kwa nchi 40 za Kiarabu na Kiislamu kwa ajili ya kushiriki kwenye mashindano ya 20 ya kimataifa ya hifdhi, kiraa na tafsiri ya Qur'ani Tukufu.
2012 Mar 04 , 17:04
Duru ya 14 ya mashindano ya Qur'ani Tukufu yamekamilika leo Jumapili huko Riyadh mji mkuu wa Saudi Arabia.
2012 Mar 04 , 17:03
Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran ameashiria hatua ya hivi karibuni ya Wamarekani kuivunjia heshima Qur'ani na kusema: 'Waislamu watajibu vikali kitendo hicho cha Wamarekani kwa kushikamana zaidi na Qur'ani'.
2012 Feb 29 , 19:09