Mwanazuoni na mwanafikra mkubwa wa Kishia wa Saudi Arabia ametoa taarifa akizitaka nchi za Kiislamu kuwaita nyumbani mabalozi wao walioko nchini Marekani kama ishara ya kupinga kitendo cha kuchomwa moto tena nakala za kitabu kitakatifu cha Qur'ani katika jimbo la Florida nchini Marekani.
2012 May 02 , 17:53
Jumuiya ya Vijana Wanamapinduzi wa Misri imetoa wito wa kufanyika maandamano makubwa ya kulaani kitendo cha kasisi wa Marekani cha kuchoma moto nakala za Qur'ani Ijumaa iliyopita na kuitaka serikali ya Misri imtimue balozi wa Marekani mjini Cairo.
2012 May 02 , 17:31
Kamati inayoandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tuzo ya Dubai imetangaza habari ya kuasisiwa hivi karibuni kituo cha nuskha za Qur'ani Tukufu zilizoandikwa kwa mkono huko Imarati, kitakachojulikana kwa jina la Sheikh Muhammad bin Rashid.
2012 May 02 , 17:03
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani vikali kitendo kiovu cha kuchomwa moto Qur’ani Tukufu katika jimbo la Florida huko Marekani.
2012 May 01 , 13:24
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali hatua ya Kasisi Terry Jones wa Kanisa la Dove World Outreach Center katika mji wa Gainsville jimboni Florida Marekani kurudia tena kitendo kichafu cha kuichoma moto Qur'ani Tukufu.
2012 May 01 , 12:42
Mashidano ya 19 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Qatar yameanza katika mji mkuu wa Qatar, Doha.
Kwa mujibu wa gazeti la Ash Sharq, raia 1500 wa Qatar pamoja na wafanyakazi wa kigeni watashiriki katika vitengo vyote vya kuhifadhi Qur'ani katika mashindano hayo.
2012 May 01 , 12:32
Mufti wa Quds na Palestina Sheikh Muhammad Hussein amelaani kitendo cha kasisi wa Marekani Terry Jones cha kuchoma moto Qur'ani Tukufu kwa mara ya pili.
2012 Apr 30 , 18:41
Kitabu cha 'Utafiti katika Historia ya Qur'ani Tukufu' ambacho kimeandikwa na Sayyid Muhammad Baqir Hujjati ni miongoni mwa vitabu vinne bora vilivyoshinda katika maonyesho ya vitabu vilivyoandikwa mwaka 2011 katika kitengo cha fasihi ya kimaanawi na historia ya kidini huko Russia.
2012 Apr 30 , 17:45
Kwa mara nyingine tena Kasisi Terry Jones wa Kanisa la Dove World Outreach Center katika mji wa Gainsville jimboni Florida Marekani, amechoma moto Qur'ani Tukufu.
2012 Apr 30 , 16:58
Hatua ya nusu fainali ya mashindano ya hifdhi ya Qur'ani yaliyopewa jina la Sultan Qaboos, ilianza nchini humo hapo jana Jumamosi.
2012 Apr 29 , 17:36
Qarii wa kimataifa kutoka Iran ametoa wito wa kutolewa mafunzo ya Qur'ani kwa watoto walemavu kwa kutumia mbinu maalumu.
2012 Apr 29 , 17:17
Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon imesimamisha masomo dhidi ya Uislamu yaliyokuwa yakitolewa katika chuo cha kijeshi cha mji wa Norfolk katika jimbo la Virginia baada ya mwanafunzi mmoja kuwasilisha mashtaka kuwa masomo hayo yanapiga vita dini ya Uislamu.
2012 Apr 28 , 19:15
Wizara ya Majumba ya Makumbusho na vituo vya kukarabati nakala zilizochaa za Qur'ani katika Umoja wa Falme za Kiarabu itatoa zawadi nakala za kale za Qur'ani Tukufu kwa nchi za Kiafrika baada ya kufanyiwa marekebisho.
2012 Apr 28 , 19:14