Kongamano la kwanza la kimataifa la muujiza wa kielimu wa Qur'ani Tukufu na Hadithi za Mtume (saw) lilianza hapo siku ya Jumapili katika Chuo Kikuu cha Bani Suweif mjini Cairo.
2012 May 08 , 14:06
Taasisi ya Kimataifa ya Abul Hudaa ya Algeria imeanzisha rasmi mpango wa kitaifa wa harakati za Qur'ani utakaohusu mafundisho na masomo ya tajwidi kote katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
2012 May 08 , 13:54
Mashindano ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani Tukufu yamepangwa kufanyika tarehe 15 na 16 Septemba katika mji wa Val d'Oise nchini Ufaransa.
2012 May 07 , 15:09
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetenga bajeti ya takribani dola nusu bilioni kwa ajili ya shughuli za Qur'ani katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.
2012 May 06 , 23:58
Masomo maalumu ya mbinu za kufundishia Qur'ani Tukufu yalianza jana Jumamosi huko Algiers mji mkuu wa Algeria.
2012 May 06 , 23:55
Chama cha mwafaka wa Kitaifa nchini Lebanon kimeleni vikali kitendo cha kuchomwa moto Qur'ani Tukufu katika jimbo la Florida nchini Marekani.
2012 May 06 , 11:26
Mashindano ya tatu ya kiraa na hifdhi ya Qur'ani Tukufu yatafanyika tarehe 3 Juni nchini Canada yakisimamiwa na Ofisi ya Kituo cha Kiislamu cha kaskazini mwa nchi hiyo.
2012 May 06 , 11:24
Chombo cha kuaminika katika Wizara ya Wakfu ya Misri kimetangaza kuwa Qur'ani kubwa ya wizara hiyo imeibwa.
2012 May 05 , 20:15
Maulamaa wa Kiislamu wa Morocco wametoa taarifa wakilaani kitendo cha kasisi Terry Jones wa Marekani cha kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu katika jimbo la Florida.
2012 May 05 , 20:14
Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Harare katika mji mkuu wa Zimbabwe kimeandaa mashindano ya Qur'ani yaliyofanyika Mei tano.
2012 May 05 , 18:22
Yassir Swalah al-Qadhi, mbunge wa Misri amewasilisha bungeni humo mswada maalumu wa sheria zinazohusiana na uchapishaji pamoja na usambazaji wa Qur'ani Tukufu pamoja na hadithi za Bwana Mtume (saw).
2012 May 05 , 18:21
Mtafiti wa masuala ya Qur'ani wa Iraq:
Maudhui ya kuvunjiwa heshima kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu, Qur'ani na kukaririwa vitendo hivyo viovu dhidi ya kitabu kitakatifu zaidi cha Waislamu na itikadi zao, vinatokana na woga wa Wamagharibi kuhusu maendeleo ya pande zote ya Waislamu na hofu yao kuhusu wimbi la wasio Waislamu kuingia katika dini hiyo.
2012 May 02 , 18:50
Mwanazuoni na mwanafikra mkubwa wa Kishia wa Saudi Arabia ametoa taarifa akizitaka nchi za Kiislamu kuwaita nyumbani mabalozi wao walioko nchini Marekani kama ishara ya kupinga kitendo cha kuchomwa moto tena nakala za kitabu kitakatifu cha Qur'ani katika jimbo la Florida nchini Marekani.
2012 May 02 , 17:53