Washindi wa mashindano ya kitaifa ya hifdhi ya Qur'ani ya nchini Jordan yaliyopewa jina la Sheikh Abdallah Ali al-Matu walienziwa na kupongezwa katika sherehe maalumu iliyofanyika hapo jana Jumatatu katika mji mkuu wa nchi hiyo Amman.
2012 May 29 , 17:15
Kongamano la kwanza la kitaifa la vituo na taasisi za hifdhi ya Qur'ani nchini Yemen lilifanyika siku ya Jumapili katika mji mkuu wa nchi hiyo Sanaa. Kongamano hilo la siku mbili lililoandaliwa na Taasisi ya Masuala ya Kheri na Maendeleo ya Yemen lilimalizika jana Jumatatu.
2012 May 29 , 17:14
Mashindano ya kwanza ya kitaifa maalumu kwa wanafunzi wa kidini nchini Iraq yamepangwa kufanyika nchini humo Juni Mosi.
2012 May 29 , 17:14
Mashindano ya kitaifa ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu yamepangwa kumalizika leo Jumatatu tarehe 28 Mei nchini Oman kwa kutangazwa majina ya wahindi.
2012 May 28 , 12:08
Muskha za Qur'ani Tukufu, tarjuma zake na mapambo mbalimbali ya kitabu hicho kitakatifu yanaonyeshwa katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu yaliyopewa jina la Jawadain (as) huko katika mji wa Kadhimain nchini Iraq.
2012 May 28 , 12:02
Baraza la Sekta ya Uchapishaji na Ufungaji ya Misri imeelezea matayarisho ya kufanyika kikao cha kuchunguza sheria mpya ya uchapishaji na usambazaji wa Qur'ani Tukufu nchini humo ambapo Sheikh wa al–Azhar anatazamiwa kushiriki.
2012 May 27 , 18:04
Kongamano la 'Qur'ani na Ahlul Beit (as) lilifanyika jana Jumamosi huko katika mji wa kihistoria wa Multan katika jimbo la Punjab nchini Pakistan kwa udhamini wa Majlisi ya Umoja wa Waislamu wa Pakistan.
2012 May 27 , 18:03
Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (bunge) amba italipa kipaumbele zaidi suala la kuimarisha utamaduni wa Qur'ani nchini.
2012 May 27 , 12:57
Waziri wa Elimu Uingereza Michael Gove amesema itakua jambo bora iwapo wafadhili wataunga mkono mpango wa kutuma nakala za Qur’ani Tukufu katika shule nchini humo.
2012 May 27 , 12:57
Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Morocco imetangaza kuwa itaandaa hatua ya mwisho ya mashindano ya kitaifa ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani Tukufu yaliyopewa jina la Mfalme Muhammad VI hapo tarehe 4 Agosti.
2012 May 26 , 18:57
Mashindano ya kitaifa ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani Tukufu yamepangwa kufanyika nchini Marekani tarehe 31 Agosti hadi 3 Septemba katika Kituo cha Mikutano cha Washington DC.
2012 May 26 , 18:57
Kuhifadhi Qur'ani utotoni ni njia muafaka zaidi na imekuwa ikitumiwa kwa muda mrefu nchini Nigeria, amesema Mhariri Mkuu wa Jarida la Al-Mizan la mjini Zaria katika jimbo la Kaduna Kaskazini mwa Nigeria.
2012 May 26 , 12:24
Mahmoud Hussein Hashimi, mwambata wa masuala ya utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Falme za Kiarabu Imarati, amesema kuwa Iran itawakilishwa hivi karibuni katika duru ya 29 ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu, Zawadi ya Dubai ambayo imepangwa kufanyika nchini humo tarehe 18 Juni.
2012 May 22 , 17:35