IQNA

Waislamu Ufaransa

Mcheza soka Muislamu amshtaki Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa

18:39 - January 17, 2024
Habari ID: 3478208
IQNA - Malalamiko ya kukashifiwa yamewasilishwa dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerald Darmanin na mchezaji mashuhuri wa sokaKarim Benzema.

Darmanin mwaka jana alisema nyota huyo wa zamani wa Real Madrid alikuwa na uhusiano na harakati ya Ikhwanul Muslimin (Mandugu Waislamu) ya Misri.

Malalamiko ya Benzema siku ya Jumanne, yaliyowasilishwa na wakili Hugues Vigier, na kuonekana na shirika la habari la AFP, yanasema matamshi haya "yanadhoofisha" heshima na sifa ya mchezaji huyo.

Katika malalamiko yake, Benzema, ambaye anachezea klabu ya Al Ittihad ya Saudia na ni Muislamu, anasema "hajawahi kuwa na uhusiano hata kidogo na shirika la Ikhwanul Muslimin, wala kujuana na yeyote anayedai kuwa mwanachama wake" .

Aliongeza: “Nafahamu ni kwa kiasi gani, kutokana na umaarufu wangu, ninatumiwa katika michezo ya kisiasa, ambayo ni ya kashfa zaidi kutokana na matukio makubwa yaliyotokea tangu Oktoba 7 yanastahili kitu tofauti kabisa na aina hii ya kauli. "

Darmanin, mwanasiasa wa mrengo wa kulia anayetaka kuwania urais wa Ufaransa, alimkosoa Benzema baada ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Ufaransa na mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or 2022 kutuma kwenye X, ambayo zamani ilijulikana kama Twitter, katikati ya Oktoba kuwaunga mkono Wapalestina wa Ukanda wa Gaza uliozingirwa ambao ni wahanga wa mashambulizi yasiyo ya haki yanayotekelezwa na Israel.

Malalamiko hayo yamewasilishwa kwa mahakama ya Cour de Justice, mahakama pekee ya Ufaransa iliyopewa mamlaka ya kuwafungulia mashitaka maafisa wa ngazi za juu katika serikali kwa makosa waliyotenda walipokuwa wakitekeleza majukumu yao.

Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria alionyesha kuunga mkono Palestina.

"Maombi yetu yote kwa wakazi wa Gaza ambao kwa mara nyingine wameathiriwa na mashambulizi yasiyo ya haki ambayo hayajawaacha wanawake wala watoto," Benzema alisema Oktoba 15.

Mshambuliaji huyo mkongwe ameshinda mataji mengi akiwa na Real Madrid, ambapo alitumia muda mwingi wa uchezaji wake, ikiwa ni pamoja na Ligi ya Uhispania, Kombe la Uhispania, Ligi ya Mabingwa ya UEFA na Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA.

3486846

Kishikizo: Karim Benzema ufaransa
captcha