IQNA

Watetezi wa Palestina

Vijana wa Yemen wapata mafunzo ya kuenda vitani kuwasaidia Wapalestina huko Gaza

21:35 - December 21, 2023
Habari ID: 3478070
IQNA - Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Ansarullah nchini Yemen imetangaza kuanza mchakato wa uhamasishaji wa vijana wanaojitolea kuenda kupigana katika vita vya Gaza pamoja na wapiganaji wa harakati za Kiislamu huko Palestina.

Huzam al-Assad, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Ansarullah amesema kwamba uhamasishaji wa jumla umeanza nchini Yemen ili kuwaunga mkono watu wa Ukanda wa Gaza.

Alisema kambi za mafunzo zimezinduliwa katika mikoa tofauti na makumi ya maelfu ya vijana wamejitolea kujifunza ujuzi wa kijeshi ili kujiunga na Jihadi huko Gaza.

Wakati masharti yanapokuwa sawa na fursa ya kuingia vitani ikijitokeza, watu wa Yemen watawasaidia wananchi wa Gaza ambao wanakabiliwa na mashambulizi ya mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel kwa msaada wa Marekani, alisema.

Assad pia alisisitiza uwezo mkubwa na wa hali ya juu wa kijeshi wa jeshi la Yemen.

Wakisisitiza uungaji mkono wao kwa watu wa Palestina na Ukanda wa Gaza, wanajeshi wa Yemen wamelenga meli kadhaa za kibiashara zinazofungamana na utawala haramu wa Israel zinazoelekea zilizokuwa zikipite kwenye Bahari Nyekundu na Mlango wa Bahari wa Bab al-Mandab hivi karibuni.

Sayyid Abdul-Malik al-Houthi, kiongozi wa Ansarullah siku ya Jumatano alisisitiza uungaji mkono wa dhati wa taifa la Yemen kwa Wapalestina na mapambano yao ya ukombozi, na kulaani baadhi ya tawala za Kiarabu ambazo zinahudumia maslahi ya utawala dhalimu Israel kwa kudungua ndege zisizo na rubani na makombora ya Yemen yaliyolenga ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).

 

4189180

 

Habari zinazohusiana
captcha