IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Kiongozi wa Ansarullah: Wazayuni wanataka kuwatenga Waislamu na Qur’ani Tukufu

9:50 - September 17, 2023
Habari ID: 3477610
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Muqawama) ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, lobi ya Wazayuni na waungaji mkono wake duniani kote wanataka kuyatenganisha mataifa ya Kiislamu na Qur'ani Tukufu na vilevile Mtume Muhammad (SAW) ili kuendeleza ajenda zao wenyewe.

Akizungumza katika hotuba iliyotangazwa na televisheni kutoka mji mkuu wa Yemen wa Sana'a siku ya Jumamosi jioni, Sayyid Abdul-Malik Badruldeen al-Houthi aliangazia kupungua kwa nguvu ya serikali ya Marekani ndani na nje ya nchi, akitoa wito kwa jamii ya Kiislamu kukumbatia mafundisho ya Kiislamu na maadili ya Mwenyezi Mungu zaidi kuliko hapo awali.

“Kadiri njama zinavyoendelezwa dhidi ya Waislamu, ndivyo tunavyopaswa kuzingatia kanuni zetu za Kiislamu na kuzigeuza changamoto kuwa fursa. Takfiri na Wazayuni wanafanya kila wawezalo kuwaweka mbali Waislamu na vyanzo vyao vya utu na uchamungu,” al-Houthi alisema.

"Kwa sasa, utawala wenye majivuno na kiburi unakusudia kupotosha jamii za wanadamu. Wameharibu maadili duniani kote ili waweze kutawala. Wanafanya hivi kwa kuwatenga Waislamu na matakatifu,” Kiongozi wa Ansarullah alisema.

Mnamo tarehe 12 Agosti, Badruldeen al-Houthi aliitaka jamii ya Kiislamu kuchukua msimamo imara dhidi ya kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu, haswa vitendo vya kuchoma Qur'ani Tukufu. Al Houthi aliyasema hayo kufuatia visa vya mara kwa mara vya kucoma moto Qur'ani Tukufu nchini Uswidi na Denmark.

Nchi kadhaa za Kiislamu zimelaani kitendo hicho cha kudhalilisha maeneo matakatifu ya Waislamu na kuwasilisha malalamiko rasmi kwa Denmark na Uswidi kupinga kuchafuliwa huko. Iran, kwa upande wake, imesema haitamtuma balozi mpya nchini Uswidi na haitamkubali mjumbe mpya wa Uswidi kama njia ya kulalamikia vitendo hivyo.

Kiongozi wa Ansarullah amesema, "Serikali za Magharibi zinapinga ukosoaji wowote wa Wazayuni, ambao unathibitisha ushawishi wa lobi zinazoiunga mkono Israel ndani ya serikali hizo.

Al Houthi pia alizikashifu baadhi ya nchi za Kiarabu na Kiislamu kwa kujiepusha kukata uhusiano na nchi ambazo Qur'ani ilitukanwa, akisema tabia hiyo inathibitisha kuwa nchi hizo zinauchukulia Uislamu kuwa jambo la kawaida.

3485193

Habari zinazohusiana
captcha