IQNA

Njia ya Haki

Mtu aliyefika Msikitini kulalamikia 'kelele' arejea nyumbani akiwa Mwislamu (+Video)

21:18 - April 26, 2023
Habari ID: 3476918
TEHRAN (IQNA) – Mzee mmoja ambaye alifika Msikitini kulalamika kuhusu kelele katika eneo hilo la ibada huko Australia hatimaye alisilimu baada ya kukaribishwa kwa ukarimu na waumini waliokuwa Msikitini hapo.

Wakati wa sherehe za Idul Fitr siku ya Jumamosi,  Hussin Goss, mwenyekiti wa Kamati ya Msikiti wa Gold Coast alitembelewa na mzee mmoja akilalamika kuhusu kile alichokiita kuwa ni kelele zilizokuwa zikitoka ndani ya Msikiti.

Mwanaume huyo, ambaye alikuwa akiishi katika nyumba ya kuwahudumia wazee, alikaribishwa kwa ukarimu na Goss ambaye alichukua nafasi hiyo kumpa chakula na kuzungumza naye kuhusu Uislamu.

Dakika chache baadaye, mtu huyo aliamua kusilimu, na alitamka shahada mbele ya Waislamu waliokuja kusherehekea Idul Fitr.

Goss ni mzee maarufu wa jamii ya Waislamu wa Gold Coast, na  amekuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislamu  kwa miaka 29.

Miaka michache iliyopita, alitunukiwa Cheti cha Shukrani na Wakfu wa Muslim Charitable Foundation kwa kusaidia "kuleta mabadiliko katika maisha ya wale wasiobahatika".

Hivi sasa kuna takriban Waislamu 10,000 wanaoishi katika eneo lote, na takriban 1200 kati yao wanahudhuria sala katika msikiti huo.

Goss alisambaza video nyingine kwenye Instagram ikimuonyesha mwanamume mwingine akikubali Uislamu katika Usiku wa Qadr, wa  tarehe 27 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

3483336

captcha