IQNA

Jinai za Israel

Kamati ya Kiislamu-Kikristo ya Al-Quds yataka Israel iadhibiwe kwa uhalifu wake

8:19 - April 11, 2023
Habari ID: 3476845
TEHRAN (IQNA)- Kamati ya Kiislamu na Kikristo inayounga mkono Quds Tukufu (Jerusalem) na Matukufu yake imetoa wito wa kuuwajibisha utawala wa Kizayuni wa Israel kwa jinai zake dhidi ya Wapalestina.

Kamati hiyo Jumapili ilitoa wito kwa waliotia saini Mkataba wa Nne wa Geneva wa 1949 na Mkataba wa The Hague wa 1954 "kuchukua majukumu yao katika kuwajibisha mamlaka ya Israel kutokana na kuendeleza uhalifu dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa na maeneo yote ya Kiislamu na Kikristo ya kidini mjini Quds.

Kamati hiyo ilisema katika taarifa yake kwamba "kuendelea uchokozi wa Israel dhidi ya watu wa Palestina na kukaidi maazimio ya kimataifa" ni "uhalifu wa kivita kwa mujibu wa sheria za kimataifa za haki za binadamu."

"Uzuiaji wa Israel kwa raia wa Palestina kutekeleza sala zao huko Al-Aqsa ni ukiukaji wa wazi wa sheria zote za kimataifa na za kibinadamu," kamati hiyo ilikariri.

Kupuuza kwa jumuiya ya kimataifa kwa jinai za Israel kumewezesha uvamizi huo kuepuka adhabu na kuendelea kufanya uhalifu huo," iliongeza.

Mapema Jumatano, tarehe 5 Aprili, wanajeshi wa Kizayuni waliwashambulia Waislamu waliokuwa katika ibada ya Itikafu ndani ya Msikiti wa Al-Aqsa na kuwalazimisha Waislamu hao kutoka nje ya eneo hilo la ibada. Katika shambulio hilo idadi kadhaa ya Wapalestina walijeruhiwa.

Video za uvamizi huo zinaonyesha wanajeshi wa Israel wakiwapiga kikatili waumini wasio na ulinzi kwa kutumia marungu na bunduki. Makumi ya Wapalestina walijeruhiwa na wengine kukamatwa katika shambulio hilo. Jina hiyo ilikaririwa tena na wanajeshi katili wa Israel.

Uchokozi huo  Israel katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani umeendelea kulaaniwa kila kona ya ulimwengu wa Kiislamu na kwingineko duniani.

/3483137

captcha