IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Ulaya nchini Ujerumani

10:48 - March 09, 2023
Habari ID: 3476681
TEHRAN (IQNA) – Toleo la 9 la Mashindano ya Qur’ani Tukufu kwa Waislamu wa barani Ulaya yataanza Ijumaa mjini Hamburg, Ujerumani.

Kwa mujibu wa Kituo cha Dar-ul-Quran cha Ujerumani, shindano hilo litaendelea hadi Jumapili, Machi 12.

Wagombea katika sehemu ya wanaume watashindana katika kategoria za kuhifadhi Qur'ani, usomaji wa Qur'ani, Adhana na ufahamu wa aya za Qur'ani.

Katika sehemu ya wanawake, kuna kategoria tatu za kuhifadhi Qur'ani, usomaji wa Tarteel na ufahamu wa aya za Qur'ani.

Fainali itafanyika Jumapili asubuhi na washindi watatangazwa na kutunukiwa katika hafla siku hiyo hiyo.

Dar-ul-Quran ya Ujerumani, yenye mafungamano na Kituo cha Kiislamu cha Hamburg kila mwaka huandaa mashindano ya Qur'ani ya Ulaya ilitangaza baadhi ya maelezo ya toleo la kumi la tukio la Qur'ani.

Dar-ul -Quran hapo awali ilisema kwamba wataalamu wa Qur'ani wanaotambuliwa kimataifa watakuwa wajumbe wa jopo la majaji.

Mashindano hayo ya kila mwaka yanalenga kukuza utamaduni na mafundisho ya Qur'ani, kubainisha na kukuza vipaji vya Qur'ani, na kuimarisha umoja katika jumuiya ya Qur'ani ya Ulaya.

 4127004

captcha