Shahi Masjid, msikiti wa karne ya 16 uliojengwa wakati wa utawala wa Sher Shah Suri ulibomolewa katika eneo la Handia la Prayagraj, Uttar Pradesh. Kulingana na idara ya kazi za umma ya Prayagraj, msikiti huo ulibomolewa ili kupanua barabara ya G T.
Cha kusikitishwa ni kwamba, imamu wa Msikiti huo, Md Babul Hussain alisema kwamba kesi hiyo iliorodheshwa katika mahakama ya chini hadi Januari 16. Lakini wakuu wa eneo wamechukua hatua ya kubomoa msikiti kabla ya kesi kusikilizwa.
Kesi hiyo ilifikishwa katika mahakama ya chini baada ya Mahakama Kuu ya Allahabad kutupilia mbali ombi la kusitisha ubomoaji huo Agosti, mwaka jana.
Klipu iliyosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu kubomolewa msikiti huo imepelekea wengi walaani utawala wa wilaya na serikali ya Uttar Pradesh kwa kitendo hicho.
3482106