IQNA

Uislamu nchini Urusi

Msikiti mkubwa zaidi Crimea, Urusi kuzinduliwa mwaka ujao

21:12 - December 29, 2022
Habari ID: 3476327
TEHRAN (IQNA) – Msikiti mkubwa zaidi katika eneo la Crimea nchini Urusi (Russia) utazinduliwa katika mji wa Simferopol mwaka ujao, afisa mmoja alisema.

Ervin Musayev, mshauri wa meya wa jiji hilo, alisema kuna maendeleo ya ujenzi wa msikiti huo sasa yamefika asilimia 85.

Alisema ujenzi huo utakamilika mwakani na Idara ya Masuala ya Dini ya Kiislamu Urusi itasimamia msikiti huo.

Alibainisha kuwa ujenzi huo ulidumu zaidi ya muda uliopangwa kutokana na janga la coronavirus.

"Tunaweza kusema kwamba mradi wa ujenzi umeingia katika awamu yake ya mwisho," Musayev alisema, akiongeza kuwa msikiti huo utakuwa zawadi kwa Waislamu wa Crimea.

Ujenzi wa msikiti huo ulianza mwaka 2015 na kwa sasa, watu 120 wanafanya kazi kwa zamu mbili ili kumaliza mradi huo.

Baada ya kukamilika, msikiti huo utakuwa na uwezo wa kukaribisha  waumini 3,000 hadi 4,000.

Crimea ni eneo ambalo liko katika pwani ya kaskazini ya Bahari Nyeusi, ambalo limekuwa chini ya udhibiti wa Urusi tangu 2014 baada ya wakazi wake wanaozungumza Kirusi kutaka kujitenga na Ukraine.

Idadi kubwa ya watu wa Crimea wanafuata Kanisa la Othodoksi, ambapo Watatari wa Crimea wanaunda jamii ya  Waislamu waliowachache.

 4110264

captcha