IQNA

Mapambano ya Wapalestina

Mash’al: Wapalestina wadumishe umoja ili wakabiline na utawala wenye kufurutu ada wa Israel

16:44 - December 26, 2022
Habari ID: 3476310
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) nje ya nchi amewatolea mwito Wapalestina wa kudumisha umoja na mshikamano baina yao ili kukabiliana na serikali mpya ya utawala haramu wa Israel inayoongozwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Khalid Mash’al amesisitiza kuwa, kuundwa Baraza la Mawaziri la Kifashisti na lenye misimamo ya kufurutu ada la Israel ni changamoto ambayo inalazimu kuweko umoja na mshikamano wa Wapalestina ili kuweza kukabiliana nayo.

Akihutubia katika mji wa Saida nchini Lebanon kwa mnasaba wa maadhimisho ya miaka 35 tangu kuasisiwa Harakati yan Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS), Khalid Mash’al ameeleza kuwa, changamoto ambayo imeletwa na baraza la mawaziri la kifashisti la Israel inahitajia kuchukuliwa maamuzi ya kishujaa na ya haraka kwa ajili ya kuhuisha umoja na mshikamano wa Wapalestina.

Kadhalika amesema kuwa, kuasisiwa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ilikuwa nukta muhimu ya kianzio katika historia katika njia ya muqawama na mapambano huko Palestina, kushikamana na misingi, amlengo matukufu, haki ya kurejea Wapalestina katika ardhi zao, kukomboa ardhi za Wapalestina na kuhakikisha kuwa mateka na wafungwa wote wa Kipalestina wanaachiliwa huru.

Amesema, baadhi ya Wazayuni wanaamini kuwa, kuundwa serikali yenye misimamo ya kufurutu ada huko Israel kunaweza kuwa ni kwa maslahi yao, lakini Wapalestina kwa kudumisha umoja na mshikamano wao wanaweza kubadilisha tishio hilo na kulifanya kuwa fursa..

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu aliyepewa jukumu la kuunda serikali mpya huko Israel alitangaza Jumatano usiku kupitia ujumbe wake wa Twitter ikiwa ni dakika chache kabla ya kumalizika makataa rasmi aliyopewa kuunda serikali, kwamba alikuwa amefikia makubaliano na vyama vya muungano kuunda baraza la mawaziri.

4109667

captcha