IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu Ufaransa

Qur'ani Tukufu yavunjiwa heshima Ufaransa, msichana wa shule avuliwa Hijabu

20:37 - October 17, 2022
Habari ID: 3475944
TEHRAN(IQNA0- Wanaharakati katika mitandao ya kijamii ya Ufaransa wamekemea vikali shambulio lililofanywa dhidi ya mwanafunzi wa Kiislamu aliyekuwa na vazi la staha la hijabu katika shule ya sekondari baada ya nakala ya Qur'ani Tukufu aliyokuwa nayo kuraruliwa na kisha akavuliwa vazii lake la Hijabu.

Vyombo vya habari vya Ufaransa vimeripoti kwamba shambulizi hilo lilimlenga mwanafunzi wa shule ya upili, John Rostand, huko Caen, kaskazini-magharibi mwa Ufaransa, ambaye alishambuliwa baaada ya vazi lake la hijabu kutupwa kwenye jaa, huku Qur'ani aliyokuwa nayo ikichanwa na kuraruliwa, jambo ambalo lilimshtua na kumuaucha bumbuazi.

Jumuiya ya Kupambana na Chuki dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa, imekaribisha msimamo wa mkurugenzi wa shule hiyo ambaye umelaani tukio hilo na kuchukua hatua za kuzuia kukaririwa kitendo hicho.

Kwa upande wake, mwandishi wa habari na mwanaharakati Siham Asbagh ameandika katika mtandao wa Twitter kwamba, "Kilichotokea ni sehemu ya kampeni ya kitaifa inayowalenga wasichana wanaovaa vazi la hijabu katika shule za sekondari za Ufaransa."

Watumiaji wengine wa mitandao ya kijamii wamesisitiza kuwa kuongezeka kwa chuki dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa kunaonyesha kuwa nchi hiyo imekuwa nchi ya taa zilizozimika.

Siku mbili zilizopita, aliyekuwa mgombea urais wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, Eric Zemmour, alizindua kampeni ya kuandamana mjini Paris na katika mitandao ya kijamii ili kupinga kile alichokiona kuwa "kuenea kwa alama na nembo za Kiislamu" katika shule za Ufaransa.

Chuki dhidi ya Uislamu na dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimeongezeka katika nchi mbalimbali za Magharibi.

Sikuu chache zilizopita genge moja la maadui wa Uislamu na la wapinzani wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran walifanya maandamano nchini Ujerumani kupinga kurushwa hewani adhana katika msikiti mmoja wa mjini Cologne.

Maadui hao wa Uislamu wamefanya maandamano hayo licha ya Msikiti huo kuomba idhini kwa manispaa ya jiji la Cologne na kuruhiwa kutumia spika kusoma adhana siku za Ijumaa.

4092361

captcha