IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Washindi wa Mashindano ya 2 ya Kimataifa ya Qur'ani la Meshkat Watangazwa

15:18 - October 15, 2022
Habari ID: 3475932
TEHRAN (IQNA) - Katika hafla ya Ijumaa, washindi wa toleo la 2 la mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Meshkat walitangazwa.

Hafla hiyo ilifanyika mjini Tehran sambamba na Milad un Nabii yaani kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW).

Zaidi ya washiriki 1,000 kutoka nchi 73 walikuwa wameshiriki katika hatua ya awali ya shindano hilo huku watu 153 wakifuzu kwa fainali ya mashindano hayo yaliyofanyika kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba 3.

Walishindana katika kategoria za usomaji wa Kurani kwa wanaume na kuhifadhi Qur'ani kwa wanaume na wanawake.

Katika kitengo cha usomaji wa wanawake, Zahra Khalil kutoka Iran alishinda tuzo ya juu huku Asi Pavnari kutoka Indonesia na Asie Ahmad Ali kutoka Nigeria wakifuata.

Katika kategoria ya kuhifadhi kwa wanaume, zawadi ya juu ilienda kwa Abdullah Ali Hassan kutoka Misri. Ayamuddin Fakhruddin kutoka Urusi na Zakaria Abu al-Aql kutoka Ubelgiji walishika nafasi ya pili na ya tatu.

Katika kitengo cha kisomo cha wanaume, Khalil Savari kutoka Iran aliibuka mshindi akifuatiwa Gholam Rasool Abbasi kutoka Afghanistan na Lotfi Kamal kutoka Indonesia walifuata.

Mshindi wa kila kitengo atatunukiwa zawadi ya pesa taslimu dola za Kimarekani 2,600 naye aliyeshika nafasi ya pili akipata US$2,300 na wa tatu $2,000.

Mashindano hayo yaliandaliwa katika sehemu mbili tofauti za kitaifa na kimataifa.

4091825

captcha