IQNA

Jumba la Makumbusho la Ustaarabu wa Kiislamu lazinduliwa mjini Istanbul

17:11 - April 09, 2022
Habari ID: 3475105
TEHRAN (IQNA)- Jumba la Makumbusho la Ustaarabu wa Kiislamu limezinduliwa kwenye uwanja wa Msikiti wa Grand Camlica, msikiti mkubwa zaidi wa Uturuki, katika wilaya ya Uskudar ya Istanbul.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alizindua jumba hilo la makumbusho siku ya Ijumaa.

Jumba hilo la makumbusho, ambalo litasimamiwa na Kurugenzi ya Majumba ya Kitaifa ya Bunge la Watu wa Uturuki (TBMM), linaonyesha mabaki mengi kutoka kwa ustaarabu wa Kiislamu.

Jumba hilo la makumbusho pia lina vifaa vya kipekee ambavyo vinafuatilia miaka 1,200 ya historia ya Kiislamu, na vingi havijawahi kuonyeshwa hapo awali.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Erdogan alisema, "Tulitambulisha lulu mpya zaidi ya Istanbul, Msikiti wa Grand Camlica, pamoja na jumba lake la sanaa, maktaba, ukumbi wa mikutano, warsha na makumbusho, kwa turathi yetu ya ustaarabu kama ishara ya utajiri wa jiografia yetu. ambayo itatumika kwa karne nyingi."

Erdogan alisema ustaarabu hukua kutokana na juhudi za pamoja za miji ambayo huongeza thamani kwa utamaduni, sanaa na sayansi.

"Msikiti wetu tulioufungua kwa ajili ya ibada yapata miaka mitatu iliyopita, ni kazi inayoongeza thamani umaridadi wa Istanbul. Jumba la Makumbusho ya Ustaarabu wa Kiislamu ni moja ya sehemu muhimu zaidi. Makumbusho haya yanawakilisha mkusanyiko wa miaka elfu moja wa ustaarabu wa Kiislamu, ambao ulileta sura mpya kabisa kwa nchi hizi," Erdogan alisema, na kuongeza kuwa kazi za thamani, ikiwa ni pamoja na vitu alivyomiliki Mtume Muhammad (SAW) na nakala za awali za Qur'ani, zinaonyeshwa. katika makumbusho.

"Natumai makumbusho yetu ya Ustaarabu wa Kiislamu ni ya manufaa kwa mji wetu, nchi yetu, na ulimwengu wetu wa utamaduni na sanaa," alisema.

Jumba hilo la makumbusho, lililojengwa katika eneo lenye ukubwa wa futi za mraba 107,639, na lina takriban vipande 800 vinavyoakisi maendeleo ya sanaa ya Kiislamu kutoka karne ya saba hadi ya 19. Jumba hilo la makumbusho lina sehemu 15 za maudhui mbali mbali.

3478415

captcha