IQNA

Mansour Hadi, kibaraka wa Saudia nchini Yemen ajiuzulu wadhifa wake

23:27 - April 07, 2022
Habari ID: 3475096
TEHRAN (IQNA)- Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa Yemen aliyejiuzulu mwenyewe na kukimbilia Saudi Arabia ametangaza rasmi kukabidhi madaraka kwa baraza jipya la urais lililoundwa karibuni.

Hadi ametangaza rasmi kuachia ngazi katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mapema leo Alkhamisi, ambapo ametangaza pia kumuuzulu makamu wake, Ali Mohsen al-Ahmar.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, baraza jipya la urais lililoundwa litasimamia masuala ya kisiasa, kijeshi na kiusalama ya Yemen katika kipindi cha mpito.

Waziri wa Habari ya Yemen amesema Dakta Rashad al-Alimeh ndiye atakayeliongoza bara hilo la mpito la urais, ambalo linatazamiwa kutangaza hali ya hatari nchini Yemen.

Jumatano ya wiki iliyopita, Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi lilianzisha mazungumzo mjini Riyadh kwa ajili ya Yemen, ambapo Abdrabbuh Mansour Hadi na makamu wake ambaye pia ni waziri mkuu hawakuhusishwa.

Ni vyema kuashiria hapa kuwa, kuanzia mwaka 1994 hadi 2012, yaani kwa muda wa miaka 18, Abdrabbuh Mansur Hadi alikuwa Makamu wa Rais Ali Abdallah Saleh wa Yemen.

Mwaka 2012 Mansour Hadi alichukua madaraka ya Yemen baada ya kupinduliwa Ali Abdallah Saleh. Aliingia madarakani katika uchaguzi wa kimaonesha ambao haukuwa na upinzani wowote.

4047405

captcha