IQNA

Kiongozi wa Jihad Islami

Wapalestina watapambana kukomboa mji wa Quds

20:37 - March 01, 2022
Habari ID: 3474991
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amesema kuwa, harakati za kupigania ukombozi wa Palestina zimepata nguvu na kuuimarika kuliko wakati wowote ule huku adui akidhoofika kuliko kipindi chochote na kwamba Wapalestina wako tayari kupambana na utawala ghasibu wa Israel kuukomboa mji wa Quds (Jerusalem) na msikiti wa Al Aqsa mjini humo.

Ziyadh al-Nakhala, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina amesema hayo katika mkutano wa "Muqawama (mapambano ya Kiislamu), Njia ya Ukombozi" ambapo sambamba na kuashiria vita vya Seif al-Quds amesisitiza kuwa, vita hivyo vilithibitisha kwamba, nguvu ya taifa la Palestina si yenye kwisha na imezidi kuimarika..

Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amesema kuwa, kubomoa na kuharibu nyumba za Wapalestina katika maeneo yote ya Ukingo wa magharibi wa Mto Jordan na kufanya mauaji dhidi ya raia wa Palestina wasio na hatia yoyote yanayofanywa na utawala haramu wa Israel ni mambo yanayowalazimu Wapalestina kutosita hata kidogo katika kuendesha vita dhidi ya adui tena wakitumia suhula na nyenzo zote.

Ziayad al-Nakhala amebainisha kwamba, adui Mzayuni ambaye alikuwa akishambulia Gaza Palestina na Lebanon na alikuwa amesonga mbele katika medani mbalimbali, lakini hivi sasa amerejea nyuma na amekimbilia kujenga ukuta wa kujilinda.

Katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni na kutokana na Wazayuni maghasibu kuzidisha jinai zao dhidi ya Wapalestina wasio na hatia kwa kutumia wanajeshi makatili wa Israel, wanamapambano wa Palestina sasa nao wameamua kutumia silaha huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds, ili kujihami mbele ya jinai za Wazayuni.

/4039560

captcha