IQNA

Taasisi ya Kiislamu yalaani kuendelea kufungwa kwa Msikiti Mkuu wa Srinagar

17:57 - February 12, 2022
Habari ID: 3474923
TEHRAN (IQNA)- Sala ya Ijumaa haikuruhusiwa kufanywa kwa wiki ya 28 mfululizo kwenye Msikiti Mkuu huko Srinagar, katika eneo la Kashmir linalozozaniwa na ambalo linatawaliwa na India

Katika taarifa yake, Taasisi  ya Anjuman Awqaf inayosimamiwa msikiti ilisema kuwa ni siku ya 28 mfululizo ya Sala ya Ijumaa haijasaliwa katika msikiti huo  na hata baada ya siku kumi za mwanzo za mwezi wa Rajab al-Murajab pia zinamalizika, lakini utawala unaendelea na msimamo wa kidikteta  wa kutowaruhusu Waislamu kutekeleza majukumu muhimu kama vile sala ya Ijumaa kwenye Masjid Srinagar, eneo kubbwa zaidi la Ibada katika eneo la Kashmir na ni kitovu cha kuhubiri Uislamu.

Taasisi  ya Anjuman Awqaf ilikariri kwamba miaka miwili na nusu ya kupigwa marufuku kwa kiongozi wa juu wa kidini wa watu wa Kashmiri, Mirwaiz-e-Kashmir Molvi Umar Farooq, kumepelekea  ashindwe kutekeleza majukumu yake ya kidini na kusema marufuku hiyo si ya haki.

Mgogoro wa Kashmir ulianza wakati Pakistan na India zilipotengana mwaka 1947 baada ya kuondoka mkoloni Muingereza ambaye alipanda mbegu za chuki baina ya mataifa hayo mawili. Wakazi wa eneo la Kashmir linalotawaliwa na India wanataka kura ya maoni iainishe hatima yao ya ama kubakia India, kupata uhuru kamili au kujiunga na Pakistan. India inapinga vikali pendekezo hilo la kura ya maoni ya kuamua hatima ya Kashmir, eneo ambalo wakazi wake wengi ni Waislamu. 

3477779

captcha