Sheikh Ahmad Ibrahim Bamba amefariki Ijumaa asubuhi mjini Kano kaskazini mwa Nigeria.
Kwa mujibu wa taarifa, mwendazake alipoteza maisha baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Kifo cha Sheikh Ibrahim Bamba kimetangazwa na mmoja wa wanae, Ahmad Muhammad Ahmad.
Sheikh Bamba aliwahi kuwa mhadhiri wa lugha ya Kiarabu katika Chuo Kikuu cha Bayero Kano kabla ya kujiuzulu na kuanzisha chuo chake cha Kiislamu alichokipatia jina la Taasisi ya Darul Hadith.