IQNA

Televisheni ya IQRA ya Misri yandaa kipindi cha kimataifa cha qiraa ya Qur'ani + Video

15:54 - November 09, 2021
Habari ID: 3474532
TEHRAN (IQNA)- Televisheni moja ya Misri inayorusha matangazo kwa njia ya sataliti ina kipindi maalumu ambacho kinajumuisha qiraa ya Qur'ani tukufu ya wasomoaji kutoka nchi mbali mbali.

Kipindi hicho cha Televisheni ya IQRA TV kinajulikana kama "Wa Rattil al-Qur'ani"  na hurushwa hewani kila wiki katika siku za Alhamisi na Ijumaa.

Wakuu wa IQRA TV wanasema lengo lao ni kustawisha usomaji Qur'ani duniani.

Mwendeshaji wa kipindi hicho ni Mus'ab Arafat, ambaye binafsi ni qarii mashuhuri nchini Misri.

Kwa mujibu wa utaratibua wa kipindi hicho qarii wa Qur'ani kutoka eneo lolote lile duniani anatuma klipu yake ya qiraa kwa njia ya WhatsApp na baada ya kuchujwa, qiraa hizo hurushwa hewani.

Watazamaji na waliotuma klipu kisha wanapata ushauri na maelekezo kuhusu njia sahihi ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani.

Kitengo kingine cha kipindi hicho kinajumuisha visa vya Qur'ani kutoka kwa Masahaba wa Mtume Muhammad SAW na wengine.

Harakati za Qur'ani ni mashuhuri sana huko Misri nchi ambayo ina wasomaji bora zaidi wa Qur'ani duniani.

4011777

captcha