IQNA

Wasichana, wavulana 1,000 waliohifadhi Qur'ani Ghaza waenziwa

22:17 - October 29, 2021
Habari ID: 3474489
TEHRAN (IQNA)- Sherehe kubwa imefanyika Jumatano usiku katika Ukanda wa Ghaza huko Palestina kuwaenzi wasichana na wavulana 1,000 ambao wamehifadhi Qur'ani hivi karibuni.

Sherehe hiyo imeandaliwa katika Kituo cha Dural Qur'ani Al Karim na Sunnah na kuhudhuriwa na wanasiasa pamoja na wawakilishi wa Wizara ya Wakfu ya Palestina.

Watoto hao 1,000 wamefanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu katika miezi ya karibuni wakati wakihudhuria darsa za Qur'ani.

Akizungumza katika mahafali hiyo, Sheikh Abdul Rahman al Jamal, mkuu wa idara ya usimamizi ya Kituo cha Dural Qur'ani Al Karim na Sunnah amewashukuru wale wote waliofanikisha harakati hiyo ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

Naye Bilal Emad, mkurugenzi wa  Kituo cha Dural Qur'ani Al Karim na Sunnah amesema kituo hicho kilianzishwa mwaka 1992 na hadi sasa kimetoa mafunzo kwa wanawak na wanaume 30,000 ambao wamehifadhi Qur'ani.

Kituo hicho kinaendesha shughuli zake kwa misaada ya wafadhili kwa lengo la kuwapa Wapalestina waishio Ghaza mafunzo ya Qur'ani Tukufu.

Tokea mwaka 2006, eneo la Ukanda wa Ghaza limekuwa chini ya mzingiro wa Israel wa nchi kavu, angani na baharini jambo ambalo limewasababishia wakaazi wa eneo hilo matatizo makubwa. Aidha utawala wa Kizayuni wa Israel umetekeleza mashambulizi kadhaa dhidi ya eneo hilo na kupelekea melefu kupoteza maisha mbali na kuharibi miundo msingi ya raia.  Pamoja na masaibu hayo yote, Wapalestina katika eneo hilo wanaendeleza shughuli zao za kidini ikiwemo kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

 

4008661

 

captcha