IQNA

Qiraa ya Qur'ani ya Sheikh Mahmoud Shahat Anwar + Video

17:44 - August 24, 2021
Habari ID: 3474221
TEHRAN (IQNA)- Qarii maarufu wa Misri Sheikh Mahmoud Shahat Anwar hivi karibuni alisoma aya za Qur'ani alipotembelea ofisi za tovuti ya Al Balad.

Katika kikao hicho alisoma Surah Quraysh kwa mbinu ya Warsh an Nafi.

Aidha akiwa hapo alizungumza kuhusu namna alivyoanza kusoma Qur'ani Tukufu huku akiashiria nafasi ya  baba na ndugu yake katika kufanikisha jitihada zake.

Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar ni mwanae marhum Sheikh Muhammad Shahat Anwar na alizwaliwa mwaka 1984.

Alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 12 kutoka kwa baba yake. Ameweza kuibuka mshindi katika mashindano mengi ya Qur'ani ya kitaifa na kimataifa. Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar  amewahi kusafiri katika nchi nyingi duniani kushiriki katika mashindano ya Qur'ani ikiwa ni pamoja na Kuwait, Iran, Afrika Kusini, Bahrain, Pakistan, Syria, Indonesia, Ufaransa, Uturuki,  Algeria na Ugiriki.

3992391

Kishikizo: anwar qiraa misri mahmoud
captcha