IQNA

Jeshi dhalimu la Israel laua shahidi Wapalestina 4 Ukingo wa Magharibi

19:56 - August 16, 2021
Habari ID: 3474195
TEHRAN (IQNA)- Askari wa utawala haramu wa Israel wamewaua shahidi vijana wanne Wapalestina kwa kuwapiga risasi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Gavana wa Jenin akisema kuwa, mabarobaro hao wanne wa Kipalestina wameuawa shahidi alfajiri ya leo Jumatatu katika kambi ya wakimbizi ya Jenin huko Ukingo wa Magharibi.

Amesema utawala huo wa Kizayuni umezuilia maiti mbili za vijana hao waliouawa. Afisa huyo wa Jenin amewataja vijana watatu miongoni mwa wanne waliouawa kuwa ni Saleh al-Ammar, Raed  Abu Seif, na Nour Jarrar.

Kwa mujibu wa takwimu, kuna walowezi wa Kizayuni wapatao 650,000 wanaoishi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds (Jerusalem) Mashariki.

Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, Ukingo wa Magharibi na Quds ni maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na hivyo ujenzi wa vitongoji ni kinyume cha sheria.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha maazimio kadhaa ya kuutaka utawala wa Kizayuni uondoke katika ardhi za Palestina ambazo unazikalia kwa mabavu.

3475513

Kishikizo: israel palestina
captcha