IQNA

Vyuo vikuu vya Iran, Ujerumani vimeandaa mafunzo ya kidini

22:43 - August 10, 2021
Habari ID: 3474178
TEHRAN (IQNA)- Kozi ya mafunzo ya kidini imeandaliwa kwa pamoja baina ya Chuo Kikuu cha Dini na Madhehebu cha Iran kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Ujerumani cha Paderborn.

Kozi itafanyika kupitia intaneti kwa lugha ya Kiingereza kutoka Agosti 31 hadi Septemba 9.

Teolojia ya Dini, mafunzo ya msingi kuhusu Maadili ya Kikristo ya Kijamii, Baraza la Pili la Vatican, na Umaanawi na Masuala ya Kiroho katika Uislamu ni mada ambazo zitajadiliwa katika kozi hiyo.

Wale walio tayari kushiriki katika kozi wanaweza kutembelea tovuti ya en.urd.ac.ir kwa habari zaidi.

Kozi hii haina malipo kwa wanafunzi wanaostahiki ambao masomo au kazi zao zinahusiana na kozi hii.

3988981

captcha