IQNA

Saudia yaanza kupokea maombi ya wanaotaka kutekeleza Ibada ya Umrah

21:23 - August 08, 2021
Habari ID: 3474172
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Hija na Umrah ya Saudi Arabia ilitangaza kwamba itakubali maombi ya Umra kuanzia Agosti 9, 2021, kwa mahujaji kutekeleza Ibada ya Hija ndogo ya Umrah.

Utoaji wa vibali utakuwa kupitia aplikesheni za simu za mkononi za "Eatmarna" na "Tawakkalna". Wizara hiyo inakusudia kupokea  Waislamu wanaotekeleza ibada ya umrah katika makundi ya watu  60,000 waliosambazwa kwa vipindi vinane vya kazi, na kuleta uwezo kwa watu milioni mbili kwa mwezi.

Naibu waziri wa Hajj na Umrah, Abdulfattah bin Sulaiman Mashat, alielezea kwamba wizara hiyo inafanya kazi kwa uratibu na mamlaka zingine kabla ya msimu ujao wa Umrah ili kuandaa  mazingira salama kwa wanaotekeleza ibada ya Hija ndego ya Umrah.

Kwa wenyeji na wakaazi, chanjo ya COVID-19 ni sharti la kutekeleza Umrah na kutembelea na kusali katika misikiti miwili mitakatifu ya Makaa na Madin. Wanaotoka nje ya ufalme wa Saudia ni lazima wawasilishe cheti rasmi cha chanjo kutoka nchi zao, pamoja na chanjo hiyo kutoka kwa orodha ya chanjo zilizoidhinishwa na Saudi Arabia. Wanaowasili Saudia pia wanapaswa kuzingatia taratibu za karantini.

Naibu waziri alisema kuwa idadi ya abiria kwenye chombo cha kusafirishia haitazidi asilimia 50 ya uwezo wake, huku wasafiri wakitakiwa kutokaribiana.

3475454/

Kishikizo: umrah saudia
captcha