Katika ujumbe wake huo, Rais Rouhani ameongeza kuwa leo dunia inakumbwa na migogoro ya kijamii, kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa na hivyo kuna haja ya kuwepo ushirikiano wa viongozi wa nchi mbali mbali ili kujikwamua kutoka katika migogoro hii. Rais wa Iran amesisitiza kuhusu ushirikiano zaidi katika kukabiliana na kirusi cha corona ili maisha yarejee katika hali ya kawaida.
Rais Rouhani ameendelea kusema kuwa Nabii Isa bin Maryam-Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake-alikuwa mtume wa amani na maelewano na mbebe bendera ya ukarimu. Ameelezea matumani yake kuwa, mwanadamu wa leo, hasa wafuasi wa Mitume wa Mwenyezi Mungu watafuata mafundisho ya mitume ili mwanadamu aweze kufikia ubora.
Rais wa Iran amewatakia viongozi wa dunia afya, salama na mafanikio ya mataifa na serikali zao.