Mwezi Machi Tunisia ilifunga mipaka yake yote ya kimataifa, ikasitisha safari baina ya miji, ikaamuru kufungwa misikiti, shule, maduka na migahawa na sheria ya kutotoka nje ikaanza kutekelezwa usiku.
Nchi hiyo ina kesi 1,048 za COVID-19 na vifo 48 hiyo ikiwa ni idadi ndogo ya maambukizi ikilinganishwa na chi jirani ya Algeria yenye kesi 10,000 na vifo zaidi ya 670.
Pamoja na kuwa misikiti na migahawa imefunguliwa, serikali ya Tunisia imesema shule zitaendelea kufungwa hadi kuanza mwaka mpya wa masomo mwezi Septemba na pia ni marufuku kuwa na mijumuiko mikubwa majumbani huku wananchi wakihimizwa kuendelea kuvaa barakoa na kutii sheria za kiafya za kuzuia maambukizi ya corona. Mipaka yakimataifa ya Tunisia inatazamiwa kufunguliwa mwishoni mwa mwezi huu wa Juni.
/3471596