IQNA

Japan yaweka vyumba vya Sala vya Waislamu katika maeneo ya kibiashara

12:56 - February 24, 2019
Habari ID: 3471851
TEHRAN (IQNA)-Kufuatia ongezeko la wageni Waislamu nchini Japan, vyumba vya Sala vya Waislamu vinawekwa katika maeneo mengi ya kibiasahra kote katika nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa, kando ya vyumba hivyo kuna eneo maalumu la kutawadha na ndani ya kila chumba kuna ishara inayoonyesha muelekeo wa qibla,

Hivi sasa kwa ujumla kuna vyumba 170 vya Waislamu kusali kote Japan na idadi hiyo inazidi kuongezeka kutokana na idadi kubwa ya Waislamu wanaotembelea nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Asia.

Kwa mujibu wa takwimu kulikuwa na watalii Waislamu wapatano 700,000 nchini Japan mwaka 2017 kutoka Malaysia na Indonesia. Ili kuzuia vyuymba hivyo kutumiwa kama eneo la kupumzika au kulala, kwa kawaida huwa vinafungwa na Mwislamu anayetaka kuswali anatakiwa kuwajulisha wasimamizi wa eneo alipo ili afunguliwe na kisha kutekeleza ibada.

Mwaka jana Japan ilizindua 'misikiti inayotembea' ambayo itatumika katika Michezo ya Olimpiki na Paralimpiki Tokyo mwaka 2020.

Aidha mwaka jana pia Shirika la Reli la Tobu mnamo Aprili Mosi ililifungua vyumba vya  Sala vya Waislamu  katika Kituo cha Tobu Nikko. Lengo la hatua hiyo lilitajwa kuwa ni kuwavutia zaidi Waislamu wanaosafiri kutoka nchi za kusini mashariki mwa Asia kama vile Malaysia na Indonesia. Nikko ni mji mdogo katika jimbo la Tochigi kaskazini mwa mji mkuu wa Japan, Tokyo.

Aidha nchini Japan hivi sasa kuna mkakati maalumu wa kuwavutia wageni Waislamu kwa kuhakikisha wanapata migahawa yenye vyakila halali katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo. Hivyo watalii wanapata fursa ya kula chakula cha Kijapani lakini ambacho ni halali.

3467983

captcha