Wanazuoni na watafiti kutoka Morocco, Mauritania, Misri, Tunisia, Ubelgiji na Algeria walihudhuria kongamano hilo ambalo lilifanyika Jumatano na Alhamisi.
Moja kati ya masuala yaliyojadiliwa kwa kina katika kongamano hilo ni utumizi wa maneno kama vile Jihad, Ummah na Qital katika lugha ya Kiarabu na lugha nyinginezo.
Washiriki pia walitoa wito kwa nchi za Waislamu duniani kuanzisha mpango mkubwa wa kutarjumu na kufasiri Qur'ani katika lugha mbali mbali.
Halikadhalika washiriku walitaka kuwepo jitihada maalumu za kukabiliana na njama za mustashriqin– (au orientalists kwa Kiingereza) ambao wamekuwa wakipotosha taswira ya Uislamu na Qur'ani.