Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yameandaliwa na Kituo cha Masomo ya Kiislamu, Chuo Kikuu cha Usmanu Danfodiyo, jimboni Sokoto kwa ushirikiano wa Kamati ya Musabaqah ya Jimbo la Kwara.
Mashindano hayo yalianza Ijumaa 4 Februari na yanatazmaiwa kuendelea hadi Jumamosi, 11 Februari katika jimbo hilo.
Mwenyekiti wa kamati andalizi ya mashindano hayo, Jaji (Mstaafu) Idris Haroon amesema yanatazamiwa kuwa na washiriki kutoka majimbo 30 ya Nigeria na yanafanyika katika Ukumbi wa Al-Hikmah.
Jaji Haroon, ambaye aliwahi kuwa Kadhi Mkuu wa Mahakama ya Kiisalmu ya Rufaa ya Jimbo la Kwara, amesema washindi watatunukiwa zawadi katika sherehe zitakazofanyika katika Uwanja wa Metropolitan.
Kwa kawaida washindo wa mashindano hayo huteuliwa kuwakilisha Nigeria katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani maeneo mbali mbali duniani.
3570130