IQNA

Seneta nchini Australia akoloslewa kwa matamshi yake dhidi ya Waislamu

20:19 - September 17, 2016
Habari ID: 3470568
Seneta Pauline Hanson wa Australia amekosolewa kwa matamshi yake yaliyojaa chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Katika hotuba yake ya kwanza bungeni Jumatano, Hanson alionya kuhusu kilo alichodai kuwa ni 'kufurika Waislamu Australia na kasha kuendelea kudai bila ushahidi kuwa, uhalifu ni mwingi katika maeneo wanamoishi Waislamu.

Akiendelea na matamshi yake yaliyojaa chuki, ameitaka Australia isitishe uhamiazi zaidi na kusema watu wanoingia nchini humo wanapaswa kufuata mila na desturi za nchi hiyo au warejee walikotoka.

Akijibu matamshi hayo, Keysar Trad, Mwenyekiti wa Jumuiya za Kiislamu Australia amesema, hotuba ya Hanson imeonyesha ujinga wake kuhusu Uislamu. Trad amesema Hanson hafahamu hata nukta a kimsingi kuhusu Uislamu na kuongeza kuwa matamshi kama hayo yatatumiwa na wenye chuki dhidi ya Uislamu kuwahujumu Waislamu.

Naye Ali Kadri, msemaji wa Baraza la Kiislamu la Queensland amesema Hanson ameonyesha kutofahamu utamaduni na Imani ya Waislamu. Aidha ameonyah kuwa matamshi kama hayo yatafanya ubaguzi kuwa kitu cha kawaida.

Waziri wa Mambo ya Nje ya Australia Julie Bishop amesema haafiki matamshi ya Hanson kuhusu Waislamu na kusema nchi hiyo imekuwa ikikaribisha wahamiaji na itaendelea kuwakaribisha wahajiri.

Waislamu wanakadiriwa kuwa ni takribani asilimia tatu ya watu wote milioni 23 nchini humo.

3460948

captcha