IQNA

Sheikh Zakzaky anazidi kuzorota kiafya, yamkini akapofuka

21:40 - July 23, 2016
Habari ID: 3470468
Mwanae mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky, Jumamosi amelalamika kuwa, wazazi wake wanazorota kiafya korokoroni na serikali imewanyima huduma za kitiba.

"Ingawa wazazi wangu hawako katika seli ya gereza, lakini waliko wanapata masaibu na hawana usalama,” Mohammad Ibrahim Zakzaky amesema katika barua kwa vyombo vya habari.

"Miezi minane iliyopita, Jeshi la Nigeria liliwaua na kuwazika kwa siri zaidi ya watu elfu moja wakiwemo ndugu zangu wawili na wakati huo huo kufyatuali risasi mama yangu mara saba huku askari wa jeshi hilo wakipelekea baba yangu kupoteza jicho lake sambamba na kumlemeza mguu na mkono. Idara ya Usalama wa Taifa Nigeria (DSS) inadai kumlinda baba yangu lakini wakati huo huo inamyima haki ya kutibiwa na madaktari wake na haki ya kupata wakili na tunaruhusiwa kuwatembelea wakati maafisa wa usalama wanapotaka,” amesema.

Ikumbukwe kuwa kati ya Desemba 12-14 mwaka 2015, Jeshi la Nigeria liliwashambulia wafuasi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria IMN katika mji wa Zaria jimboni Kaduna kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi lilidai kuwa wafuasi wa IMN walikuwa na jama ya kutoaka kumuua Mkuu wa Jeshi la Nigeria, madai ambayo yamekanusha vikali na wafuasi wa harakati hiyo. Waislamu Zaidi ya 1,000 wanaripotiwa kuuawa katika mauaji yaliyotekelezwa na Jeshi la Nigeria na baada ya hapo kumkamata Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria akiwa pamoja na mke wake.

Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Kiislamu ya Uingereza imetangaza kuwa faili la mauaji ya Waislamu katika mji wa Zaria nchini Nigeria limewasilishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu huko The Hague nchini Uholanzi.

Taarifa iliyotolewa mwezi Machi na Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Kiislamu ya Uingereza (IHRC) imesema faili la mashambulizi na mauaji yaliyofanywa na jeshi la Nigeria dhidi ya Waislamu wa mji wa Zaria limepelekwa Hague katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, uhalifu uliofanywa na jeshi la Nigeria katika kipindi cha tarehe 12 hadi 14 Disemba katika mji wa Zaria dhidi ya Waisalmu ni jinai dhidi ya binadamu na kuna udharura wa kutolewa amri ya uchunguzi wa mahakama ya ICC kuhusu uhalifu huo.

IHRC imesisitiza kuwa ushahidi uliopo unathibitisha kwamba mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la Nigeria dhidi ya Waislamu wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Zakzaky yalikuwa yamepangwa.

3470211

captcha