IQNA

Wakuu wa Nigeria kumfungulia mashtaka Sheikh Zakzaky

14:35 - December 21, 2015
Habari ID: 3467870
Maafisa wa Nigeria wamesema kuwa Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ambaye alitiwa nguvuni na jeshi huku familia na wafuasi wake wakichukuliwa hatua kali za jeshi na kusababisha umwagaji damu watashtakiwa.

Jumamosi wiki hii Nasir al Rufai, Gavana wa jimbo la Kaduna la kaskazini magharibi mwa Nigeria ambako Sheikh Zakzaky alitiwa mbaroni akiwa nyumbani kwake katika mji wa Zaria wiki iliyopita, amesema kuwa kiongozi huyo atafunguliwa mashtaka kwa kosa lolote atakalokuwa ametenda.

Itakumbukwa kuwa vikosi vya Nigeria Jumapili iliyopita viliivamia nyumba ya Sheikh Ibrahim Zakzaky Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria na kumtia mbaroni baada ya ya jeshi hilo kuua raia waliojaribu kumlinda kiongozi huyo wa kidini akiwemo mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wa harakati hiyo na msemaji wa harakati hiyo.

Siku hiyo jeshi la Nigeria liliishambulia Husainiyyah ya Baqiyyatullah katika mji wa Zaria pamoja na nyumba ya Sheikh Ibrahim Zakzaky na kuwaua mamia ya Waislamu kwa kisingizio kwamba Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ilikula njama ya kutaka kumuua mkuu wa jeshi na kufunga njia kwa ajili ya shughuli za mijumuiko ya kidini ya harakati hiyo. Baadhi ya ripoti zinasema kuwa, idadi ya waliouawa katika shambulio hilo la jeshi la Nigeria inafikia Waislamu elfu mbili.

3467578

Kishikizo: zakzaky nigeria waislamu
captcha