IQNA

Njama ya Saudia katika mauaji ya Waislamu Nigeria

16:18 - December 20, 2015
Habari ID: 3467471
Mkuu wa Jumuiya ya Maulamaa wa Kisuni wa Iraq amefichua mkono wa Saudi Arabia katika mauaji yaliyofanywa na jeshi la Nigeria dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika mji wa Zaria.

Sheikh Khalid al Mulla amesema kabla ya mauaji ya mamia ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Nigeria kanali ya televisheni ya al Wisal ya Saudi Arabia ilitoa ripoti ya kichochezi kuhusu kasi ya kuenea madhehebu ya Shia nchini humo na baada ya hapo ulimwengu ulishuhudia maafa ya mauaji makubwa ya Waislamu hao.

Sheikh al Mulla amesema Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na Chuo Kikuu cha al Azhar nchini Misri ambacho ndiyo marejeo makuu ya Waislamu wa madhehebu ya Suni zinapaswa kulaani na kuchukua msimamo wa wazi kuhusu mauaji ya Waislamu wa Nigeria.

Sheikh Khalid al Mulla pia amekosoa muungano eti wa kupambana na ugaidi unaoongozwa na Saudi Arabia na kusema umeanzishwa kwa ajili ya kutatiza zaidi hali ya Mashariki ya Kati kwa sababu Saudia wa waitifaki wake ndio waungaji mkono wa ugaidi katika eneo hilo.

Ni vyema kukumbusha hapa kuwa Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na waitifaki wao wa Magharibi hususan Marekani ndio walioanzisha na kufadhili kundi la kigaidi la Daesh kwa ajili ya kuiondoa madarakani serikali halali ya Syria.

3467215

Kishikizo: nigeria waislamu zakzaky
captcha