Imearifiwa kuwa watu waliokuwa na silaha wanaoaminika kuwa wafuasi wa kundi la kigaidi linalojiita Ansar Din walivamia Hoteli ya Byblos katika mji wa Sevare mapema Ijumaa kwa lengo la kuwachukua mateka raia wa nchi za Magharibi katika hoteli hiyo.
Hoteli hiyo pia inatumiwana wafanyakazi wa Kikosi cha Umoja wa Mataifa Mali MINUSMA. Katika taarifa, MINUSMA imesema wafanyakazi wake kadhaa wameuawa katika hujuma hiyo. Maafisa wa jeshi la Mali wameivamia hoteli hiyo na kuwanusuru raia kadhaa wa kigeni.
Kundi la Ansar Din linjidai kuwa la Kiislamu lakini linaeneza ugaidi na itikadi potofu na limetumia pengo la madaraka nchini Mali kueneza satwa katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.../mh