IQNA

Iran kushiriki mashindano ya Qur’ani nchini Sudan

12:26 - July 14, 2015
Habari ID: 3327976
Iran itashiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu nchini Sudan.

Ali Assadi Sefyar atawakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashindano hayo ya kimataifa yatakayofanyika Khartoum, mji mkuu wa Sudan mwezi Desemba.
Wawakilishi wa nchi za Kiislamu na zisizokuwa za Kiislamu watashiriki katika mashindano hayo ya kuhifadhi Qur’ani kikamilifu.
Sefyar ambaye ni hafidh wa Qur’ani kikamilifu alikuwa wa pili katika mashindano ya 36 ya kitaifa ya Qur’ani nchini Iran kwa ajili ya vijana mwaka jana.
Sudan ni nchi ya Kiarabu katika Bonde la Nile kaskaziini mwa Afrika na asilimia 97 ya wakaazi wake ni Waislamu.../mh

3327943

captcha