Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Russia TASS, tamasha hilo linafanyika kwa mnasaba wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani yalianza Julai 11.
Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Mamufti wa Russia Rushan Abbyasov amesema tamasha hilo litafanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Moscow kwa muda wa siku saba.
Wanazuoni wa kidini, watarjumi, wakiwemo kutoka Iran, Jamhuri ya Azerbaijan, Kazakhstan, Tajikistan, Uturuki na India wanatazamia kuhutubia tamasha hilo.
Washiriki wataonyesha kazi zao za Kiislamu kuhusu Qur’ani Tukufu, filamu, habari, fasihi ya kisayansi, vitabu vya wanazuoni wa Kiislamu na vitabu vilivyotarjumiwa..../mh